Nafasi za kazi Serikalini kupitia UTUMISHI (Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) hutangazwa rasmi kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania wenye sifa stahiki kuomba ajira katika taasisi na idara mbalimbali za umma. Kupitia mfumo wa kuajiri wa kielektroniki (Recruitment Portal), waombaji wa nafasi hizi huwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kwa uwazi na ushindani wa haki.
Bonyeza hizo link hapo chini kupakua pdf za matangazo ya ajira mpya serikalini:
- TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA
- TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA MANISPAA YA SINGIDA
- TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI
UTUMISHI huhakikisha kuwa ajira Serikalini zinatolewa kwa kuzingatia vigezo vya kitaaluma, uadilifu, na usawa kwa makundi yote ya kijamii. Kwa kawaida, nafasi hizi hutangazwa mara kwa mara kwenye tovuti ya UTUMISHI na magazeti ya Serikali, zikiambatana na masharti ya kazi, sifa zinazohitajika, na maelekezo ya jinsi ya kutuma maombi. Mfumo huu husaidia kuweka uwazi katika mchakato wa ajira Serikalini na kutoa fursa kwa Watanzania wote kushiriki katika ujenzi wa taifa kupitia utumishi wa umma.
Mapendekezo ya mhariri: