wa waombaji wote wanaotaka kujiunga na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (Institute of Finance Management – IFM), kupata Fomu ya Kujiunga na Chuo cha IFM Dar es Salaam ni hatua ya msingi katika mchakato wa udahili. IFM ni miongoni mwa vyuo vikuu vinavyoongoza Tanzania katika fani za fedha, uhasibu, benki, bima, kodi na teknolojia ya habari, na hutumia mfumo wa maombi ya mtandaoni ili kurahisisha zoezi la kuomba masomo.
Tofauti na zamani ambapo fomu zilipatikana kwa njia ya karatasi, kwa sasa fomu ya kujiunga na Chuo cha IFM Dar es Salaam hupatikana rasmi kupitia mfumo wa maombi ya chuo (Online Application System).
Fomu ya Kujiunga na Chuo cha IFM Inapatikana Wapi?
Fomu ya kujiunga na IFM Dar es Salaam inapatikana mtandaoni pekee kupitia mfumo rasmi wa maombi ya IFM unaopatikana katika anuani ifuatayo:
👉 https://ems.ifm.ac.tz/application
Kupitia mfumo huu, mwombaji anaweza:
- Kujisajili (Create account) kwa kutumia barua pepe na namba ya simu
- Kujaza fomu ya maombi ya udahili kwa ngazi husika
- Kuchagua kozi/programu anayotaka kusoma
- Kupakia nyaraka muhimu kama vyeti vya elimu, cheti cha kuzaliwa na picha
- Kufuatilia hatua za maombi hadi kupokea majibu ya udahili
Hatua za Kuomba Kupitia Mfumo wa IFM
Ili kupata na kujaza fomu ya kujiunga na Chuo cha IFM Dar es Salaam, mwombaji anatakiwa kufuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti ya mfumo wa maombi: https://ems.ifm.ac.tz/application
- Jisajili kwa mara ya kwanza au ingia (login) kama una akaunti
- Jaza taarifa zako binafsi na za kielimu kwa usahihi
- Chagua programu/kozi unayoomba
- Hakiki taarifa zako kisha wasilisha maombi
Ni muhimu kuhakikisha taarifa zote zinaingizwa kwa usahihi ili kuepuka kuchelewa au kukataliwa kwa maombi.
Soma pia: