Kupoteza cheti cha kuzaliwa ni jambo linaloweza kumpata mtu yeyote. Hii nyaraka ni muhimu sana kwa matumizi mbalimbali kama vile kuomba kitambulisho cha taifa (NIDA), pasipoti, huduma za kijamii, au hata usajili wa shule na kazi. Kwa bahati nzuri, nchini Tanzania kuna utaratibu rasmi unaokuwezesha kupata nakala mpya ya cheti cha kuzaliwa (duplicate) kama ulichopoteza. Katika makala hii, tutakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kufanikisha jambo hili mwaka 2025.
Hatua za Kufuatilia Cheti Kipya cha Kuzaliwa
1. Tayarisha Barua ya Kuthibitisha Upotevu
Kabla ya kuanza mchakato, unatakiwa kuwa na barua ya kupoteza nyaraka kutoka kituo cha polisi (Police Loss Report). Barua hii itatumika kama ushahidi kwamba cheti kilipotea.
2. Nenda Ofisi ya RITA (Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini)
Tembelea ofisi yoyote ya RITA iliyo karibu na wewe. Kama uko mbali, unaweza pia kutumia tovuti ya RITA https://www.rita.go.tz.
3. Jaza Fomu Maalum
Katika ofisi ya RITA au mtandaoni, utapewa fomu ya kuomba duplicate ya cheti cha kuzaliwa. Utahitajika kujaza taarifa kama:
- Jina kamili la aliyezaliwa
- Tarehe ya kuzaliwa
- Mahali pa kuzaliwa
- Majina ya wazazi
4. Ambatanisha Nyaraka Muhimu
Pamoja na fomu, utaambatanisha:
- Nakala ya kitambulisho cha taifa (au cha mzazi kama mwombaji ni mtoto)
- Barua ya kupoteza kutoka polisi
- Ushahidi wa uhusiano kama mzazi anamuombea mtoto
5. Lipa Ada ya Huduma
Kwa mwaka 2025, ada ya kupata duplicate ya cheti cha kuzaliwa ni TZS 3,000 hadi 5,000 kutegemeana na eneo na njia ya malipo. Malipo yanaweza kufanyika benki au kwa mfumo wa GePG (Government e-Payment Gateway).
6. Subiri Muda wa Kuchakata
Baada ya kuwasilisha maombi na nyaraka zote, RITA huchukua kati ya siku 5 hadi 14 kuchakata ombi lako. Utapewa taarifa lini na wapi uende kuchukua cheti chako kipya.
Kupata cheti cha kuzaliwa kilichopotea si kazi ngumu kama unafuatilia taratibu sahihi. Hakikisha unakuwa na nyaraka zote zinazotakiwa na kufuata utaratibu wa RITA kwa usahihi. Cheti hiki ni muhimu kwa matumizi mbalimbali ya kiserikali, hivyo ni vyema kukihifadhi vizuri mara baada ya kukipata.
Soma pia: