Tazama vituo vya kufanyia Usaili Ajira za Jeshi la Polisi 2025. Baada ya kutangazwa kwa orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili wa ajira za polisi, pia jeshi la polisi limetoa orodha ya vituo ambavyo usaili huo utafanyika kwa Tanzania Bara na visiwa (Zanzibar).
Kwa Tanzania Bara, wenye Elimu ya Kidato cha nne na cha sita watafanyia usaili kwenye ofisi za makamanda wa mikoa walipoombea na kwa wenye Elimu ya Astashahada, stashahada na Shahada watafanyia usaili kwenye uwanja wa polisi kilwa (Police Barrack) mkoani Dar es salaam.
Kwa Zanzibar, wote wenye Elimu ya kidato cha nne, sita, astashahada, stashahada na Shahada waliopo unguja watafanyia usaili ofisi ya mkuu wa polisi na kwa waliopo pemba watafanyia usaili katika ofisi ya mkuu wa polisi mkoa wa pemba chakechake