Jeshi la Polisi Tanzania limetangaza nafasi mpya za kujiunga na jeshi hilo kwa mwaka 2026/2027, hivyo kutoa fursa kwa Watanzania wenye sifa na vigezo vinavyohitajika kuomba nafasi hizo na kupata nafasi ya kulitumikia taifa kupitia chombo hicho cha ulinzi na usalama.
Tangazo hili linatoa fursa kwa vijana wenye nia ya kufanya kazi katika Jeshi la Polisi na kushiriki katika kulinda maisha ya watu, mali zao, kudumisha amani na kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa.
Sifa na vigezo vya kujiunga
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa na mwenye asili ya Tanzania.
b) Wazazi wake wawe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa na mwenye asili ya
Tanzania.
c) Awe amehitimu kidato cha nne mwaka 2024 au 2025 na kidato cha sita mwaka
2025 au 2026.
d) Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada wawe
na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
e) Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka
la nne (Division I – IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la nne (Division
IV) wawe na ufaulu wa alama (Points) 26 hadi 28.
f) Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza mpaka
la tatu (Division I – III).
g) Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi
30.
h) Awe na urefu usiopungua futi tano na inchi sita (5’6”) kwa wanaume, na futi
tano inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
i) Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya
vitambulisho vya taifa (NIDA).
j) Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza kwa ufasaha.
k) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
l) Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto/watoto.
m) Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya za aina yoyote.
n) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
o) Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
p) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
q) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye
usaili.
r) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
s) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.