Katika mfumo wa malipo ya mishahara nchini Tanzania, wafanyakazi wa taasisi za umma (Serikalini) na sekta mbalimbali Binafsi wanakutana na makato kadhaa ya lazima kwenye mshahara wao. Makato haya ni sehemu ya mwendelezo wa kuhakikisha wafanyakazi wanapata mafao ya kustaafu, bima ya ulemavu / vifo, na pia kuchangia kodi ya mapato. Kuelewa jinsi makato haya yanavyofanya kazi ni muhimu kwa kila mfanyakazi anayetaka kujua “take home” yake. Makala hii inaeleza kwa undani kuhusu makato ya PAYE, makato ya NSSF/PSSSF, na bima ya Afya NHIF.
Mchanganuo wa makato ya Mshahara wa Muajiriwa wa Serikali PAYE, NSSF/PSSSF na NHIF
1. PAYE (Pay-As-You-Earn)
PAYE ni kodi ya mapato ya mshahara ambayo mwajiri hukata kutoka kwa mshahara wako na kuwasilisha kwa Mamlaka ya Kodi (TRA).
- Mfumo wa PAYE nchini Tanzania ni wa progressive, yaani kiwango cha kodi hukua kadri kipato kinavyoongezeka
- Kiwango cha chini cha kodi ni 0% kwa mshahara mdogo sana: kwa mujibu wa vyanzo, pale mshahara wa mwezi haizidi TZS 270,000 hakuna kodi ya PAYE
Kiwango cha kodi hukua:
- 270,001 – 520,000 TZS → 8% ya kiasi kinacho zidi 270,000.
- 520,001 – 760,000 TZS → mshahara wa juu zaidi hupimwa kwa kiwango cha 20% (kwenye sehemu zinazozidi).
- 760,001 – 1,000,000 TZS → kiwango cha kodi ni 25% kwenye sehemu inayozidi 760,000.
- Zaidi ya 1,000,000 TZS → kiwango cha 30% kwenye sehemu ya mshahara inayozidi.
NB: Makato ya PAYE hufanyika baada ya Mshahara kukatwa makato ya NSSF/PSSF
2. NSSF / PSSSF (Mfuko wa Hifadhi ya Jamii)
Hapa ni sehemu ya “bima ya uzeeni / pensheni” ambayo inasaidia kutoa mafao ya pensheni, bima ya ulemavu, vifo, na ya muda mfupi kama kuzaa, ajira kupotea, nk.
A. NSSF (National Social Security Fund)
- Kiwango cha mchango ni jumla 20% ya mshahara wa mfanyakazi: 10% kutoka mfanyakazi na 10% kutoka mwajiri.
- Michango hulipwa kila mwezi, na mwajiri ni lazima awolee hilo.
Faida zinazotokana na mchango wa NSSF ni pamoja na: pensheni ya kustaafu, pensheni ya ulemavu, pensheni kwa warithi (survivor), mafao ya uhamisho wa ajira, bima ya kumbukumbu ya mazishi, nk.
B. PSSSF (Public Service Social Security Fund)
- Kwa watumishi wa sekta ya umma (serikali), mchango wa hifadhi ya jamii hufanywa kupitia PSSSF.
- Kiwango cha mchango kwa PSSSF ni asilimia 20% ya mshahara wa mfanyakazi: 5% hutolewa na mfanyakazi na 15% hulipwa na mwajiri (serikali).
- Sheria za PSSSF (Public Service Social Security Fund Act) zinaeleza kuwa hii ni mchango wa lazima.
- Faida za PSSSF ni sawa na zile za hifadhi ya jamii: pensheni, ulemavu, vifo, na faida za muda mfupi.
Bima ya Afya
- Mfuko wa Bima jumla ya Makato ni 6% ya Mshahara huku Muajiri huchangia 3% na Muajiriwa ambae ndio mfanyakazi huchangia 3%
- Mfuko huu wa bima unalenga kulinda wafanyakazi iwapo watajeruhi, kupata ulemavu au vifo kutokana na ajira.
Makato ya mshahara (PAYE, NSSF / PSSSF, na bima) ni sehemu ya msingi wa mfumo wa malipo nchini Tanzania. Ingawa yanaweza kupunguza kiasi cha pesa unachopokea kila mwezi (net pay), makato haya ni muhimu kwa usalama wa kifedha wa baadaye, kulinda wafanyakazi na kusaidia serikali kukamilisha majukumu yake ya huduma za umma. Kuelewa makato haya ni ujuzi muhimu kwa kila mfanyakazi – na ni mojawapo ya hatua za umuhimu kwa usimamizi wa fedha zako binafsi.
Soma pia: