Hatua kwa Hatua Jinsi ya kuangalia majina ya waliochaguliwa kidato cha tano (Form Five Selection) 2025/26. Form Five Selections ni mchakato muhimu unaoratibiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa ajili ya kuwachagua wanafunzi waliohitimu kidato cha nne kujiunga na kidato cha tano au vyuo vya kati nchini Tanzania. Mchakato huu hufuata baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (CSEE), na unalenga kuwapatia wanafunzi nafasi katika shule au vyuo kulingana na ufaulu wao, machaguo waliyofanya kupitia mfumo wa Selform, na nafasi zilizopo.

Jinsi ya kuangalia Form five selection: Hatua kwa HatUA
Fatisha hatua hizo hapo chini kuangalia majina ya waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka 2025/26 form five selection:
- Kwanza tembelea Mfumo wa Selformform tamisemi >> BONYEZA HAPA KUINGIA MFUMO
- Utakuta kibox kimeandikwa FIRST SELECTION na sehemu nyingine Bonyeza hapo.
- Utachagua mkoa uliopo shule yako, Mfano shule yako ni Manzese secondary basi utachagua Dar es salaam
- Pia utachagua wilaya ambayo shule yako inapatikana
- Ukishachagua wilaya zitakuja shule zote za secondary ambazo zinapatikana kwenye hiyo wilaya, Utachagulia shule yako.
- Selection zitafunguka, Utaona jina la mwanafunzi, tahasusi, na Shule ya kidato cha Tano aliyopangiwa.
Soma pia: Form five selection 2025/26