Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba kuajiriwa nafasi za kazi katika ofisi za TAKUKURU Wilaya kama inavyoonekana hapo chini
AFISA UCHUNGUZI (NAFASI 250)
Sifa za Mwombaji:
Muombaji awe na angalau elimu ya shahada ya kwanza iliyotolewa na chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika moja ya fani zifuatazo: Uhasibu, Usimamizi wa Biashara, Usanifu wa Majengo, Ukadiriji wa Majengo (Quantity Surveying), Uhandisi wa Usindikaji wa Kemikali, Maendeleo ya Jamii, Sayansi ya Kompyuta/TEHAMA, Uhandisi wa Ujenzi, Uchumi na Mipango, Uhandisi wa Umeme, Lishe na Sayansi ya Chakula. Usimamizi wa Rasilimali Watu. Usimamizi na Tathmini ya Ardhi, Sheria, Uhandisi wa Mitambo, Uhandisi wa Mafuta na Gesi, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Miradi, Ushauri Nasaha, Utawala wa Umma, Mahusiano ya Umma/Mawasiliano ya Umma, Usimamizi wa Kumbukumbu, Sayansi ya Michezo/Elimu ya Viungo, Takwimu, na Uhandisi wa Maji.
- Muombaji awe na ufaulu wa kuanzia daraja la pili la chini (lower second class).
- Waombaji waliosajiliwa na Bodi za Kitaaluma watapewa kipaumbele zaidi.
Sifa zingine:
- Waombaji wasiwe wamefika umri wa miaka 29 kufikia May, 2026
MCHUNGUZI MSAIDIZI (NAFASI 250)
Sifa za Mwombaji:
Awe na angalau cheti au astashahada kutoka kwenye shule, vyuo vinavyotambulika na serikali kwenye moja kati ya fani zifuatazo
Ulinzi (Security Skills):
Lazima awe na “Basic Technical Certificate/Technical Certificate /Diploma in Wildlife Management and Law Enforcement, or Basic Peoples Militia Training” kutoka taasisi inayotambuliwa nchini Tanzania, pamoja na uzoefu katika ulinzi.
Ufundi wa Magari / Panel Beating / Upakaji Rangi (NVA/NTA Ngazi ya 3- 4):
Lazima awe na cheti cha NVA/NTA Ngazi ya 3-4 katika fani ya ufundi wa magari, pamoja na Uzoefu na ujuzi wa vitendo katika matengenezo.
Ujuzi wa Udereva (Madereva Daraja “C”):
Lazima awe na leseni halali ya udereva Daraja C, rekodi safi ya udereva, na uzoefu unaothibitika katika uendeshaji salama wa vyombo vya moto.
Huduma kwa Wateja / Msaidizi wa Ofisi (Office Attendant):
Lazima awe na Cheti katika fani yoyote, akiwa na uzoefu wa kuhudumia wateja na uwezo wa kusaidia shughuli za ofisi.
Msaidizi wa Uhasibu (Assistant Accountant):
Lazima awe na diploma inayotambuliwa katika fani ya uhasibu pamoja na uelewa wa taratibu na mifumo ya fedha za umma.
Masomo ya Ukatibu (Katibu Muhtasi):
Lazima awe na diploma ya masomo ya ukatibu Muhtasi, akiwa na umahiri katika usimamizi wa ofisi, mawasiliano, na matumizi ya vifaa vya TEHAMA.
Fundi wa Kompyuta (Ukarabati wa Kompyuta):
Lazima awe na cheti au diploma ya ufundi katika matengenezo ya kompyuta, akiwa na Uzoefu unaothibitika katika uchunguzi na ukarabati wa vifaa(hardware), mitandao, na matatizo ya msingi ya programu (software).
Fundi wa Mashine za Ofisi (Ukarabati wa Vifaa vya Ofisi):
Lazima awe na mafunzo ya kiufundi pamoja na uwezo wa kufunga, kutunza, na kufanya matengnezo ya mashine za ofisi (K.M printer, Photocopier na Scanner).
Sifa zingine:
Mwombaji ni lazima awe raia Tanzania na mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
- Mwombaji lazima awe mtu mwenye uadilifu wa hali ya juu.
- Mwombaji asiwe na rekodi yoyote ya uhalifu.
- Awe tayari kufanya kazi katika wilaya yoyote ya Tanzania Bara
- Mwombaji lazima awasilishe nakala za vyeti halisi zilizothibitishwa. Mwombaji atakayewasilisha vyeti vya kughushi au kutoa taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.
- Mtu yeyote ambaye amefukuzwa au ameachishwa kazi kutoka katika Utumishi wa Umma kwa sababu yoyote ile hastahili kuwasilisha maombi.
- Mtumishi wa Umma anayeomba nafasi hii lazima apitishe maombi yake kwa mwajiri wake.
- Mwombaji lazima aambatishe nakala za hati zilizothibitishwa zifuatazo:
- Vyeti vya Shahada/Stashahada ya Juu na Nakala ya Matokeo ya Masomo
- Vyeti vya Kidato cha IV na Kidato cha VI
- Cheti cha Darasa la Saba
- Vyeti vya Kitaalamu (pale inapohusika)
- Cheti cha Kuzaliwa
- Picha moja ya ukubwa wa pasipoti iliyopigwa hivi karibuni.
- Vyeti vya kitaaluma vilivyotolewa na taasisi za elimu za nje ya Tanzania lazima vithibitishwe na mamlaka husika za udhibiti hapa nchini (TCU, NACTVET, NECTA).
- Mwombaji lazima aambatishe Wasifu (CV), ukijumuisha maelezo kuhusu uzoefu wa kazi, anuani ya makazi, anuani ya posta, baruapepe, na nambari ya simu.
- Mwombaji lazima awasilishe majina na mawasiliano ya kuaminika ya wadhamini watatu.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au nambari ya utambulisho wa NIDA ni lazima.
- Barua za uthibitisho, sehemu ya nakala ya matokeo ya masomo, na slipu ya matokeo ya mitihani hazitakubaliwa.
- Barua ya maombi lazima iandikwe kwa mkono kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza. 14. Maombi yasiyojumuisha nyaraka zote zinazohitajika hayatazingatiwa.
- Waombaji watakaopita mchujo wa awali tu ndiyo watakaojulishwa.
JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI
Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielekitroniki wa ajira wa TAKUKURU ambao anuani yake ni: ajira.pccb.go.tz na si vinginevyo. Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kwa mkono hayatapokelewa.
BONYEZA HAPA KU DOWNLOAD PDF TANGAZO LA KAZI TAKUKURU PCB 2026
Barua za maombi ya ajira ziandikwe kwa Anuanwi;
Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
Mtaa wa Jamhuri,
S.L.P. 1291,
41101 DODOMA.
MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: Tarehe 03 Mei, 2026