Tamisemi imetoa muda wa wahitimu wa kidato cha Nne (Form Four) wanaotarajia kujiunga na kidato cha Tano au Form five kubadilisha combination – Tahasusi kwa mwaka wa masomo 2026. Hii inasaidia baada ya matokeo kutoka mwanafunzi anakuwa tayari ameshajua ni masomo yapi amefaulu hivo itasaidia kupata shule kwa urahisi zaidi.
JIUNGE GROUP LA KUPATA AJIRA
BONYEZA HAPA
Kubadilisha Tahasusi (combination) kidato cha Tano 2026: Hatua kwa hatua
Hatua kwa hatua jinsi ya kubadilisha tahasusi (combination) kidato cha tano kwa mwaka 2026 kupitia tamisemi selform:
- Tembelea website ya kubadilishia tahasusi ama bonyeza hapa >> https://selform.tamisemi.go.tz/CandidateRegistration/
- Kwakua ni mara ya kwanza hivi utaweka namba ya mtihani ya mwanafunzi kama ilivyoonyeshwa kwenye mfano
- Kisha utaverify na kurudi kwenye login
- Baada ya kuingia, utaona sehemu kama:
- Chagua tahasusi unazotaka (unaweza kuweka priorities 1–10).
- Bofya SAVE & NEXT au Save & Go Back ili kuendelea au kurekebisha.
- Ukimaliza, thibitisha na subiri confirmation. Unaweza kupakua au kuchapisha fomu yako.
Mapaka hapo utakuwa umefanikiwa kubadilisha tahasusi, sasa unaweza kusubiria kupangiwa shule.