Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetoa taarifa leo Jumatatu, tarehe 1 Desemba 2025, kuhusu matokeo ya awamu ya tatu ya ugawaji wa mikopo na ruzuku kwa mwaka wa masomo 2025/2026, ambapo jumla ya wanafunzi 21,851 wamepata ufadhili. Takwimu hizi zinahusisha waombaji wa rufaa pamoja na wanafunzi wapya na wanaoendelea kama inavyoelezwa hapa chini:
JIUNGE GROUP LA KUPATA AJIRA
BONYEZA HAPA
- Wanafunzi 6,487 wa mwaka wa kwanza wa shahada wameidhinishwa kupata mikopo kupitia dirisha la rufaa yenye jumla ya TZS 21.5 bilioni.
- Wanafunzi 2,611 wa shahada ya awali wamekubaliwa kupokea mikopo kupitia mfumo wa maombi ya kawaida yenye thamani ya TZS 8.3 bilioni.
- Wanafunzi 11,419 wanaoendelea na masomo (FTCs) wamepata mikopo kwa mara ya kwanza yenye jumla ya TZS 37.2 bilioni.
- Wanafunzi 1,235 wa kozi za stashahada za mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS 3.2 bilioni.
- Wanafunzi 31 wapya wanaofadhiliwa kupitia ‘Samia Scholarship’ wamepewa ruzuku yenye jumla ya TZS 5 bilioni.
- Wanafunzi 68 wa masomo ya juu (postgraduate), wakiwemo 53 wa Uzamili na 15 wa Uzamivu, wamegawiwa kiasi cha TZS milioni 361.7.
Bodi imesisitiza kuwa mchakato wa ugawaji mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea na malipo kwa waliokwishaingia vyuoni utaendelea hadi ukamilike.
KUPATA MAJINA TAFADHARI TEMBELEA ACCOUNT YAKO YA SIPA
Soma pia: