Viwango vya mishahara ya wauguzi hutofautiana kulingana na uzoefu, kiwango cha elimu, eneo la kazi, na sera za mwajiri. Kwa ujumla, wauguzi wenye shahada ya juu au waliobobea katika fani maalum hupata mishahara ya juu zaidi ikilinganishwa na wale walio na mafunzo ya msingi. Katika maeneo ya mijini au hospitali za kibinafsi, mishahara huwa juu zaidi kuliko katika maeneo ya vijijini au vituo vya afya vya serikali.
Hata hivyo, licha ya mchango mkubwa wa wauguzi katika sekta ya afya, changamoto bado zipo kuhusu kulipwa kwa haki na kwa wakati, jambo linaloathiri motisha na utendaji wao kazini. Serikali na taasisi binafsi zina jukumu la kuhakikisha wauguzi wanalipwa mishahara stahiki ili kuboresha huduma za afya kwa jamii.
Viwango vya mishahara ya wauguzi
Tukizungumzia viwango vya mishahara ya wauguzi inategemea na Kiwango cha Elimu, Kuna wauguzi wa Astashahada (certificate), Stashahada (Diploma) na Shahada (Degree) leo tutazungumzia kwa viwango vyote vya Elimu.
Viwango vya mishahara ya wauguzi wa Astashahada (Certificate)
Muuguzi aliyesoma hadi Astashahada yaani certificate of nursing and midwifery atalipwa kwa ngaziya mshahara wa TGTS B, na mgawanyiko wa hela kama ufuatavyo:
TGTS B
TGTS B.1 | 479,000 |
TGTS B.2 | 489,000 |
TGTS B.3 | 499,000 |
TGTS B.4 | 509,000 |
TGTS B.5 | 519,000 |
TGTS B.6 | 529,000 |
Viwango vya mishahara ya wauguzi wa Stashahada (Diploma)
Hii ngazi ya pili kwenye sekta ya uuguzi, Muuguzi aliyesoma hadi stashahada (Diploma) mshahara wake unakomea kwenye TGTS C, na mgawanyiko wa hela kama ufuatavyo:
TGTS C
TGTS C.1 | 590,000 |
TGTS C.2 | 603,000 |
TGTS C.3 | 616,000 |
TGTS C.4 | 629,000 |
TGTS C.5 | 642,000 |
TGTS C.6 | 655,000 |
TGTS C.7 | 668,000 |
Viwango vya mishahara ya wauguzi wa Shahada (Degree)
Hii ndio ngazi ya juu kwenye sekta ya wauguzi, muuguzi mwenye elimu ya shahada yaani Bachelor degree in Nursing and Midwifery. Ngazi yake ya mshahara ni TGTS D na mgawanyiko wa mshahara ni kama ifuatavyo:
TGTS D
TGTS D.1 | 771,000 |
TGTS D.2 | 788,000 |
TGTS D.3 | 805,000 |
TGTS D.4 | 822,000 |
TGTS D.5 | 839,000 |
TGTS D.6 | 856,000 |
TGTS D.7 | 873,000 |