Bei ya tiketi na Viingilio mechi ya simba na Stellenbosch FC katika kombe la shirikisho CAFCCL. Viingilio vya mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF (CAF Confederation Cup) kati ya Simba SC na Stellenbosch FC itakayochezwa Jumapili, Aprili 20, 2025, kwenye Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar, vimetangazwa rasmi. Viingilio hivyo ni kama ifuatavyo:
- VIP A: Tsh 40,000
- VIP B (Uruzi): Tsh 20,000
- Mzunguko Orbit: Tsh 10,000
Tiketi zinapatikana kupitia vituo mbalimbali vya mauzo nchini kote. Kwa mfano, Stellenbosch FC inatoa tiketi za mechi zao kupitia Webtickets na maduka ya Pick n Pay nchini Afrika Kusini . Kwa upande wa Simba SC, mashabiki wanashauriwa kufuatilia taarifa rasmi kutoka klabu na vyombo vya habari ili kujua vituo vya mauzo na njia nyingine za kupata tiketi.