Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anawaarifu waombaji wote wa ajira kupitia mfumo wa ajira.zimamoto.go.tz kwamba zoezi la usaili litaanza tarehe 15 Disemba, 2025 hadi 20 Disemba, 2025 kuanzia saa 1:00 asubuhi, kulingana na makundi yafuatayo:
- Waombaji wenye elimu ya kidato cha nne watafanyiwa usaili tarehe 15 Disemba, 2025 saa 1:00 asubuhi katika mikoa waliyotaja wakati wa kuwasilisha maombi yao.
- Waombaji wa Shahada na taaluma mbalimbali watafanyiwa usaili katika Ukumbi wa Andengenye, Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Dodoma, kuanzia tarehe 15 hadi 20 Disemba, 2025 saa 1:00 asubuhi, kwa mpangilio ufuatao:a) Taaluma ya michezo (sportsmen) watapimwa kuanzia tarehe 15–17 Disemba, 2025. Makundi yamegawanywa katika A, B na C; kundi A litafanya usaili tarehe 15, kundi B tarehe 16 na kundi C tarehe 17 Disemba, 2025. Orodha ya makundi na tarehe imewekwa kwenye kiambatanisho kilichopo kwenye tovuti.b) Emergency Medical Technician na Nursing watapimwa tarehe 18 Disemba, 2025.c) Taaluma ya uzamiaji (Diver) watapimwa tarehe 19 Disemba, 2025.d) Fire Fighting and Rescue Profession, Avionics, Civil Engineer, Data Scientist, Motor Vehicle Mechanics, Quantity Surveyor, Marine Engineer, Oil and Gas Engineer, Office Management Secretary, ICT Technician, ICT Network Technician na Madereva watapimwa tarehe 20 Disemba, 2025.
Maelekezo kwa washiriki wa usaili:
i. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye kituo chake cha usaili siku na tarehe alizopangiwa.
ii. Wote wanapaswa kuja na vyeti halisi walivyotumia kuombea ajira, ikiwemo vya kidato cha nne, kidato cha sita, taaluma, cheti cha kuzaliwa, pamoja na kitambulisho cha taifa au namba ya NIDA.
iii. Waombaji wa nafasi ya Udereva wanatakiwa pia kuwasilisha leseni ya udereva ya Daraja E.
iv. Gharama za usafiri, chakula na malazi zinabebwa na msailiwa wakati wote wa usaili.
Soma pia: