Sifa na Vigezo vya kusoma CPA nchini Tanzania ni moja ya mada muhimu kwa wanafunzi na wataalamu wanaotaka kujenga msingi thabiti katika taaluma ya uhasibu. Kozi ya CPA inayosimamiwa na NBAA (National Board of Accountants and Auditors Tanzania) ndiyo ngazi ya juu ya taaluma ya uhasibu nchini, na imegawanywa katika hatua tofauti kuanzia Accounting Technician hadi Professional Levels.
Sifa na Vigezo mbalimbali vinavyohitajika wakati wa Kusoma CPA
Hapa tumeelezea Sifa na vigezo vyote muhimu ya kujiunga, kuanzia ngazi ya ATEC Level I hadi Final Level ya Professional Examinations—ili kukusaidia kupanga vizuri safari yako ya kuwa mhasibu aliyesajiliwa.
1. Accounting Technician – ATEC LEVEL I
Hii ndiyo ngazi ya kuanzia kwa wanaotaka kujenga msingi wa taaluma ya uhasibu. Kwa mujibu wa Vigezo na Sifa za Kusoma CPA Tanzania, muombaji wa ATEC I anatakiwa kuwa na angalau moja ya sifa zifuatazo:
Sifa za Kujiunga na ATEC Level I
- CSEE yenye credit 3 pamoja na ufaulu wa Hisabati na Kiingereza.
- NABE Stage I & II, ufaulu wa masomo manne pamoja na cheti cha sekondari.
- ACSEE, ufaulu wa principal moja na subsidiary katika masomo yanayohusika, lakini lazima uwe umefaulu Hisabati na Kiingereza O-level.
- Cheti cha mwaka mmoja kutoka taasisi inayotambulika, pamoja na ufaulu wa Kiingereza na Hisabati O-level kabla ya kupata cheti.
- Vyeti vingine vinavyotambuliwa na Bodi ya NBAA pale inapofaa.
2. Accounting Technician – ATEC LEVEL II
Kwa muombaji wa ATEC II, masharti yanakuwa juu zaidi, yakionyesha maendeleo ya kitaaluma.
Sifa za Kujiunga na ATEC Level II
- Awe na Barua ya ufaulu ya Accounting Technician Level I
- Awe na A-Level masomo ya biashara na ufaulu wa principal mbili.
- Cheti cha Accounting (NTA Level 4)
- Diploma ya miaka miwili (bila Accounting kama somo kuu) – NTA Level 6
- Wenye A-Level waliofanya Bookkeeping na Commerce na ufaulu mzuri.
3. PROFESSIONAL EXAMINATIONS – CPA Levels
Hapa ndipo safari ya kweli ya kupata cheti cha CPA Tanzania inaanza. Professional Examinations zinajumuisha:
- Foundation Level (Knowledge & Skills)
- Intermediate Level (Skills & Analysis)
- Final Level (Analysis, Application & Evaluation)
A. Foundation Level – Knowledge and Skills
Muombaji anatakiwa kuwa na moja ya sifa hizi:
- ATEC II Certificate
- Diploma ya miaka miwili katika Accounting au Accounting & Finance – NTA Level 6
- Shahada yoyote kutoka taasisi inayotambulika (isipokuwa Accounting).
NB: Misamaha hutolewa somo kwa somo kulingana na masomo ya mwanafunzi.
B. Intermediate Level – Skills and Analysis
Sifa za kujiunga:
- Awe na ufaulu wa NBAA Foundation Level
- Shahada yenye Accounting kama somo kuu au Accounting & Finance kutoka taasisi inayotambulika.
C. Final Level – Analysis, Application & Evaluation
Kuingia katika ngazi ya mwisho ya CPA, muombaji anatakiwa kuwa na:
- Ufaulu wa Intermediate Level
Ngazi hii ndiyo hatua ya mwisho kabla ya kutunukiwa cheti cha Certified Public Accountant (CPA).
Kuelewa Vigezo na Sifa za Kusoma CPA Tanzania ni hatua muhimu kwa yeyote anayetamani kuwa mhasibu wa kitaaluma nchini. Kutoka ngazi ya ATEC hadi CPA Final, kila hatua imewekewa masharti mahsusi ili kuhakikisha wahitimu wanakuwa na ujuzi, weledi, na uwezo wa kufanya kazi kwa viwango vya kimataifa.
Ikiwa unatafuta kozi yenye thamani kubwa katika soko la ajira, CPA ni mojawapo ya chaguo bora zaidi.
Soma pia: Ada na Gharama za kusoma CPA 2025