VETA Tazania imetangaza mafunzo ya muda mfupi katika mradi ambao utakuwa unatoa fani za Agro-Mechanics, Umwagiliaji (Irrigation) na Teknolojia ya Uhifadhi wa Mazao Baada ya Mavuno (Post-Harvest Technology). Mafunzo yatatolewa kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza itaanza tarehe 19 Januari, 2026.
Fani Zitakazotolewa VETA
Mafunzo ya ufundi stadi yatatolewa katika fani zifuatazo:
- Ufundi wa Zana za Kilimo (Agro-Mechanics)
- Umwagiliaji (Irrigation)
- Teknolojia ya Kuhifadhi Mazao Baada ya Mavuno (Post-Harvest Technology)
Mikoa Inayostahili Kuomba VETA
Waombaji kutoka mikoa ifuatayo wanahimizwa kuomba:
Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Lindi, Morogoro, Pwani, Ruvuma, Njombe, Iringa, Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Katavi, Kigoma, Rukwa, Mbeya, Songwe na Kagera.
Sifa za Kujiunga VETA
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:
- Awe Mtanzania
- Awe na umri wa miaka 15 au zaidi
- Awe na elimu ya msingi au kuendelea
Utaratibu wa Kuomba VETA
Maombi yatafanyika kwa njia zifuatazo:
- Mtandaoni (VETA Online Application) au kupitia tovuti ya VETA: www.veta.go.tz
- Kwa kuchukua fomu (Hardcopy) katika vyuo vya VETA vya Kihonda, Manyara, Mpanda na Arusha (Oljjoro).
Maelekezo Muhimu:
- Fomu zote zitatolewa bure na zitajazwa kwa usahihi.
- Mwombaji anatakiwa kuambatanisha cheti cha kuzaliwa na vyeti vya elimu aliyonayo.
- Fomu iliyojazwa irejeshwe chuoni husika au kutumwa mtandaoni kupitia mfumo wa maombi.
Bonyeza hapa kuangalia tangazo katika PDF
Kipindi cha Maombi VETA
| Tukio | Tarehe |
|---|---|
| Kuanza kupokea fomu | 19 Desemba, 2025 |
| Mwisho wa kupokea maombi | 2 Januari, 2026 |
Ada na Gharama za Mafunzo VETA
- Ada ya mafunzo italipwa na AGRA kupitia Mradi wa YEFFA.
- Mafunzo ni bure kwa waombaji waliokidhi vigezo.
Wanawake na watu wenye mahitaji maalum wanahimizwa sana kuomba.
Mawasiliano VETA
Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi, wasiliana na:
VETA Makao Makuu
Barabara ya VETA, Tambukareli
S.L.P 802, Dodoma
Baruapepe: info@veta.go.tz | pr@veta.go.tz
Simu: 0755 26 74 89.
Soma pia: