Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetangaza fursa za kujiunga kwa kujitaolea mwaka 2026, likiwaalika vijana wa Kitanzania wenye sifa stahiki kushiriki mafunzo ya uzalendo, ujasiri na stadi za maisha zitakazowasaidia kujitegemea na kulitumikia taifa. Nafasi hizi zinalenga kuwajenga vijana kimaadili, kimwili na kiakili kupitia mafunzo ya kijeshi ya awali pamoja na shughuli za uzalishaji, huku zikitoa fursa ya kuongeza nidhamu, uzalendo na mshikamano wa kitaifa kwa washiriki watakaokidhi vigezo vilivyotangazwa rasmi.
Utaratibu wa Vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na Mafunzo hayo, unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi. Aidha, vijana wenye taaluma za Diploma in Information Technology, Diploma in Business Information Systems, Diploma in Computer Science, Diploma in Information and Communication technology (ICT),
Diploma in Cyber Security and Digital Forensics, Bachelor of Science in Computer Science, Bachelor of Science in Information Technology, Bachelor of Science in Computer Engineering, Bachelor of Science in Business Information Technology, Bachelor of Science in Cyber Security and Digital Forensics, Bachelor of Science in Computer Networks and information Security Engineering na Vijana wenye Vipaji vya Michezo mbalimbali, wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kupitia Mikoa yao.
Usaili wa Vijana hao kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 26 Jan 2026 kwa Mikoa yote Tanzania Bara na Visiwani. Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye Makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia tarehe 27 Februari 2026 hadi 04 Machi 2026.
Aidha, Jeshi la Kujenga Taifa linapenda kuwataarifu Vijana watakaopata fursa hiyo kuwa halitoi ajira, pia halihusiki kuwatafutia ajira katika Asasi, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyo ya Kiserikali, bali hutoa Mafunzo yatakayosaidia Vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza Mkataba wao na JKT.