Shirika la Ndege Air Tanzania imetangaza nafasi 102 za kazi kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha huduma zake kwa abiria wa ndani na nje ya nchi. Nafasi hizi hulenga Watanzania wenye sifa stahiki, maadili mema na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira yenye ushindani na uwajibikaji mkubwa. Kupitia ajira hizi, Air Tanzania inalenga kuimarisha rasilimali watu, kukuza vipaji vya ndani na kuchangia maendeleo ya sekta ya usafiri wa anga pamoja na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Nafasi 102 za Kazi kutoka Shirika la Ndege Air Tanzania
| /N | Jina La Tangazo | Idadi Ya Nafasi | Mahali | Tarehe Ya Mwisho |
|---|---|---|---|---|
| 1 | Msaidizi Wa Huduma Za Upishi Daraja La Pili | Nafasi 5 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 2 | Afisa Huduma Za Upishi Daraja La Kwanza | Nafasi 4 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 3 | Afisa Wa Kumbukumbu Daraja La Pili | Nafasi 1 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 4 | Afisa Rasilimali Watu Daraja La Pili | Nafasi 3 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 5 | Afisa Utawala Daraja La Pili | Nafasi 1 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 6 | Msaidizi Wa Uhasibu Daraja La Pili | Nafasi 1 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 7 | Afisa Wa Uhasibu Daraja La Pili | Nafasi 2 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 8 | Mhasibu Daraja La Pili | Nafasi 5 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 9 | Dereva Daraja La Pili | Nafasi 4 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 10 | Msaidizi Wa Ununuzi Daraja La Pili | Nafasi 5 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 11 | Afisa Ununuzi Daraja La Pili | Nafasi 2 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 12 | Afisa Uhusiano Wa Umma Daraja La Pili | Nafasi 2 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 13 | Afisa Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano Daraja La Pili (Usimamizi Wa Mifumo) | Nafasi 1 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 14 | Afisa Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano Daraja La Pili (Usimamizi Wa Mitandao) | Nafasi 1 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 15 | Afisa Teknolojia Ya Habari Na Mawasiliano Daraja La Pili (Uendelezaji Wa Programu) | Nafasi 2 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 16 | Mkaguzi Wa Ndani Daraja La Pili | Nafasi 1 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 17 | Mkaguzi Mkuu Wa Ndani | Nafasi 2 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 18 | Msaidizi Wa Mauzo Na Masoko Daraja La Pili (Mauzo Na Uhifadhi) | Nafasi 12 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 19 | Afisa Mauzo Na Masoko Daraja La Pili (Mauzo Na Uhifadhi) | Nafasi 10 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 20 | Afisa Mauzo Na Masoko Daraja La Kwanza (Mtendaji Wa Mauzo) | Nafasi 5 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 21 | Afisa Mauzo Na Masoko Daraja La Kwanza (Masoko Ya Kidijitali Na Ubunifu Wa Maudhui) | Nafasi 3 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
| 22 | Afisa Mauzo Na Masoko Daraja La Pili (Mtendaji Wa Mauzo) | Nafasi 6 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/02/2026 |
| 23 | Afisa Ratiba Za Wahudumu Wa Ndege Daraja La Pili | Nafasi 8 | Dar Es Salaam, Tanzania | 12/01/2026 |
Jinsi ya Kutuma maombi ya Nafasi za kazi Shirika la Ndege Tanzania ATCL
Maombi yote yaandikwe kwa barua ya kingereza iliyosainiwa kisha itummwe kupitia anuani:
Managing Director & CEO,
Air Tanzania Company Limited,
P.O. Box 543,
Dar es Salaam.Maombi yote yawasilishwe kupitia Mfumo wa Ajira Online (Recruitment Portal) kwa kutumia anuani ifuatayo:
https://recruitment.atcl.co.tz
Mwisho wa kutuma maombi niĀ tarehe 12 Januari, 2026.
BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI NAFASI ZA KAZI AIR TANZANIA
Soma pia: Nafasi za kazi uhamiaji