Serikalini ya Tanzania imetangaza Ajira Mpya zaidi ya 17,710 za walimu, Afya, Kilimo, Ufugaji na Uhandisi kupitia MDAs na LGAs ajira portal
MDAs (Ministries, Departments and Agencies) ni taasisi za serikali kuu zinazohusika na utekelezaji wa sera, mipango na sheria za taifa. Kila wizara (Ministry) inasimamia sekta fulani kama elimu, afya au kilimo, huku idara na wakala (Departments and Agencies) wakitekeleza majukumu maalum chini ya wizara hizo.
LGAs (Local Government Authorities) ni mamlaka za serikali za mitaa zinazohusika na utoaji wa huduma za kijamii moja kwa moja kwa wananchi katika maeneo yao. Hizi ni pamoja na halmashauri za miji, manispaa, na wilaya.