Baraza la usimamizi wa Mitihani ya Taifa limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya shule ya msingi yaani matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2025 na kuorodhesha shule za sekondari walizopangiwa vijana waliofaulu kuendelea na elimu ya sekondari.
Baraza la mitihani ya Taifa NECTA linahimiza wazazi, walezi na wanafunzi kufatilia matokeo yao haraka iwezekanavyo ili kuweza kujua shule gani wamepangiwa.

Hatua za kuangalia matokeo ya darasa la saba na shule walizopangiwa 2025
Unaweza kutazama matokeo ya darasa la saba kama ifutavyo:
- Fungua tovuti ya baraza la mitihani Tanzania NECTA necta.go.tz
- Kisha Bonyeza kiunganishi cha Matokeo
- Chagua kada ya Elimu ambayo ni PSLE
- Utachagua Mkoa na Wilaya uliyosoma
- Kisha malizia kwa kuchagua shule ya msingi uliyohitimu.
- Utpata orodha nzima ya matokeo kutoka shule uliyosoma.