Wazazi, walimu, na wanafunzi wengi nchini Tanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua matokeo ya darasa la saba 2025 yatatoka lini. Kwa mujibu wa taarifa za awali, Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) linatarajia kutangaza matokeo hayo mwezi wa Oktoba 2025. Hii imekuwa ni desturi ya kila mwaka, ambapo baada ya mitihani kukamilika mwezi Septemba, NECTA huanza mchakato wa usahihishaji na uhakiki wa majibu kabla ya kuyatangaza rasmi.
Kwa Nini Matokeo Hutoka Oktoba?
Mchakato wa usahihishaji wa mitihani unachukua muda kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaoshiriki katika Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba (PSLE). NECTA huhakikisha kila karatasi ya mtihani inakaguliwa kwa umakini ili kutoa matokeo sahihi na yenye haki kwa kila mwanafunzi. Kwa sababu hiyo, mwezi wa Oktoba umekuwa kipindi cha kawaida cha kutangaza matokeo haya muhimu.
Matokeo ya Darasa la Saba ni hatua muhimu katika safari ya elimu ya mtoto. Ndiyo yanayotumika kuchagua shule za sekondari ambazo wanafunzi watajiunga nazo mwaka 2026. Hivyo, ni kipindi cha msisimko mkubwa kwa familia nyingi nchini
Kwa sasa, NECTA bado haijatangaza tarehe rasmi ya kutoka kwa matokeo ya Darasa la Saba 2025, lakini kwa kuzingatia utaratibu wa miaka iliyopita, matokeo yanatarajiwa Oktoba 2025. Wazazi na wanafunzi wanashauriwa kufuatilia taarifa rasmi kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) kupitia tovuti na vyombo vya habari vya serikali.
Soma pia: