Kusafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kwa basi ni mojawapo ya safari ndefu zaidi lakini pia ya kuvutia nchini Tanzania. Ikiwa unatafuta usafiri wa uhakika, nafuu na wenye huduma bora, mabasi ya Dar kwenda Mwanza yanakupa fursa ya kusafiri salama huku ukifurahia mandhari ya Tanzania.
Aina ya Mabasi Yanayotoa Huduma Dar – Mwanza
Kwa sababu ya umbali (takribani kilomita 1,200), kampuni nyingi hutoa mabasi ya luxury na semi-luxury kwa ajili ya safari hii ndefu. Baadhi ya kampuni zinazojulikana ni:
- Katarama Luxury
- Ally’s Star bus
- Happy Nation
- Isamilo
- ABC Upper Class
- Lucky Star
- Princes Shabaha
- Green Star Express
- Kambas
- Princes Munaa
- Najmunisa
- Simiyu Express
- Igembensabo
- Master City Limited
- Best line
Ratiba ya Mabasi Dar kwenda Mwanza
Safari nyingi huanza kati ya saa 11 alfajiri hadi saa 2 asubuhi, kwa sababu ni safari ya saa 18–20 kutegemea na hali ya barabara na kituo cha mwisho.
Vidokezo Muhimu:
- Weka tiketi mapema kwa sababu safari ni moja tu kwa siku kwa mabasi mengi
- Fika kituoni mapema ili usikose basi
- Beba chakula kidogo na maji kwa ajili ya safari ndefu
Nauli za Mabasi Dar to Mwanza
Bei ya tiketi inategemea aina ya huduma:
- Semi-luxury: Tsh 70,000 – 90,000/=
- Luxury/Executive Class: Tsh 110,000 – 180,000
Baadhi ya mabasi hutoa huduma za Wi-Fi, viti vya kulala (reclining seats), televisheni na hata milo midogo.
Vituo Vikuu vya Kuanzia na Kufikia
Dar es Salaam:
- Ubungo Bus Terminal (UBT) – Kituo kikuu kwa mabasi yote ya mikoani
Mwanza:
- Nyegezi Bus Terminal
- Buzuruga (kwa baadhi ya kampuni)
Kwa Nini Usafiri kwa Basi?
- Nafuu kuliko ndege
- Unaweza kubeba mizigo zaidi bila gharama kubwa
- Fursa ya kuona miji mbalimbali kama Dodoma, Singida, Shinyanga njiani.
Mapendekezo ya Mhariri: