Kilimanjaro ni mkoa wa kaskazini wa Tanzania unaojivunia mlima maarufu duniani – Mlima Kilimanjaro. Mji wa Moshi, ambao ni kitovu cha utalii wa kanda hiyo, unapokea maelfu ya wageni kila mwaka. Kwa wasafiri wa ndani, safari ya kwa mabasi ya Dar kwenda Kilimanjaro ni njia bora, nafuu na yenye mandhari ya kuvutia. Iwe unakwenda kwa shughuli za kibiashara, familia au utalii, blog hii itakupa mwongozo wote wa safari yako ya mwaka 2025.
Kampuni Maarufu za Mabasi ya Dar kwenda Kilimanjaro
Kuna kampuni nyingi zenye mabasi ya kisasa yanayotoa huduma ya kila siku kati ya Dar es Salaam na Kilimanjaro (Moshi, Himo, au Holili). Kampuni hizi zinatoa huduma za Luxury, VIP, na Semi-Luxury:
- Kilimanjaro Express
- Aboud Bus
- Tahmeed Coach
- Shabiby Line
- Marangu
- BM Coach
Baadhi ya mabasi haya yana huduma kama Wi-Fi, AC, viti vya kulala, USB chargers, na televisheni kwa kila abiria.
Ratiba ya Mabasi na Muda wa Safari
Mabasi mengi huondoka mapema:
- Asubuhi kuanzia saa 12:00 hadi saa 2:00 kutoka:
- Magufuli Bus Terminal
- Ubungo Mjini Bus Terminal
Muda wa safari:
- Masaa 10 hadi 13, kutegemea na hali ya barabara, msongamano na idadi ya vituo vya kati (Morogoro, Chalinze, Same n.k.).
Nauli za Mabasi ya Dar kwenda Kilimanjaro
Bei ya tiketi inatofautiana kulingana na aina ya huduma:
- Semi-Luxury: TZS 60,000 – 85,000
- Luxury/VIP: TZS 90,000 – 110,000
Kusafiri kwa mabasi ya Dar kwenda Kilimanjaro ni chaguo sahihi kwa wale wanaotaka kuunganisha gharama nafuu, usalama na uzoefu mzuri wa barabarani. Ukiandaa safari yako kwa umakini, kuchagua kampuni bora na kujiandaa vizuri, utajikuta ukiwasili Moshi au maeneo ya jirani ukiwa na tabasamu. Karibu Kaskazini!
Soma Pia;