Ikiwa wewe ni mtumiaji wa N-Card, basi unajua thamani ya kuwa na salio la kutosha kwa ajili ya kununua tiketi za mpira, kuingia kwenye matukio ya michezo, au huduma nyingine zinazohusiana.
Kwa bahati nzuri, kuongeza salio kwenye N-Card ni rahisi kupitia huduma kuu za kifedha kwa simu nchini Tanzania: M-Pesa (Vodacom), Mixx by Yas (Tigo Pesa), Airtel Money, na sasa pia Halopesa.
Katika muongozo huu, tutaeleza hatua kwa hatua jinsi ya kuongeza salio kwenye akaunti yako ya N-Card kwa kila mtandao.

Jinsi ya Kuongeza Salio N-Card kwa M-Pesa (Vodacom)
- Piga
*150*00# - Chagua
4> Lipa bili - Chagua
4> Ingiza namba ya kampuni - Weka namba ya kampuni:
009009 - Weka Wallet ID (namba ya N-Card)
- Weka kiasi unachotaka kuweka
- Ingiza namba ya siri (PIN)
- Chagua
1> Kukubali
Jinsi ya Kuongeza Salio N-Card kwa Mixx by Yas (Tigo Pesa)
- Piga
*150*01# - Chagua
4> Lipa bili - Chagua
3> Ingiza namba ya kampuni - Weka namba ya kampuni:
009009 - Andika Wallet ID ya N-Card yako
- Weka kiasi
- Ingiza namba ya siri (PIN)
- Chagua
1> Kukubali
Jinsi ya Kuongeza Salio N-Card kwa Airtel Money
- Piga
*150*60# - Chagua
5> Lipa bili - Chagua
4> Ingiza namba ya kampuni - Andika namba ya kampuni:
009009 - Weka kiasi cha pesa unachotaka kuweka
- Ingiza Wallet ID ya akaunti yako ya N-Card
- Ingiza namba ya siri (PIN)
- Chagua
1> Kukubali
Jinsi ya Kuongeza Salio N-Card kwa Halopesa
- Piga
*150*88# - Chagua
4> Lipa bili - Chagua
3> Ingiza namba ya kampuni - Andika namba ya kampuni:
009009 - Weka Wallet ID ya akaunti yako ya N-Card
- Ingiza kiasi
- Andika namba ya siri (PIN)
- Thibitisha kwa kuchagua
1> Kukubali
Kwa kutumia simu yako ya mkononi na mojawapo ya huduma hizi za kifedha, unaweza kuongeza salio kwenye akaunti yako ya N-Card kwa urahisi na haraka. Hii inakuwezesha kuendelea kufurahia huduma kama kununua tiketi za michezo na nyinginezo bila kikwazo. Hakikisha unafuata hatua sahihi kulingana na mtandao unaotumia.
Soma pia: Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira kwa Kutumia N-Card