Jinsi ya Kununua Vipande vya UTT AMIS kwa Njia Rahisi (M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money, CRDB, NMB) UTT AMIS (Unit Trust of Tanzania – Asset Management and Investor Services) ni taasisi inayowezesha Watanzania wa kipato cha aina zote kuwekeza kwa njia rahisi kupitia mifuko ya pamoja. Mojawapo ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara ni: “Nawezaje kununua vipande vya UTT?” Makala hii itakuongoza hatua kwa hatua jinsi ya kununua vipande kwa kutumia simu au benki maarufu Tanzania.
Jinsi ya Kununua Vipande kwa Njia ya Simu
1. Kupitia M-Pesa (Vodacom)
Fuata hatua hizi:
- Piga *150*00# kisha bonyeza Call.
- Chagua 4. Lipa kwa M-Pesa.
- Chagua 5. Orodha zaidi.
- Chagua 3. Michango ya uanachama.
- Chagua UTTAMIS.
- Weka Kumbukumbu namba (Hii ni akaunti namba ya mfuko wako wa UTT, mfano: namba ya mkataba).
- Weka kiasi unachotaka kuwekeza.
- Weka Namba yako ya siri ya M-Pesa ili kukamilisha malipo.
2. Kupitia Tigo Pesa
- Piga *150*01#.
- Chagua 4. Lipa Bili.
- Chagua 3. Ingiza namba ya kampuni.
- Weka namba ya kampuni ya UTT AMIS: 800100.
- Weka namba ya kumbukumbu (namba ya akaunti yako/mfuko).
- Weka kiasi cha fedha.
- Thibitisha kwa kuweka namba ya siri ya Tigo Pesa.
3. Kupitia Airtel Money
- Piga *150*60#.
- Chagua 5. Lipa Bili.
- Chagua 1. Kwa kampuni.
- Chagua 1. Ingiza namba ya kampuni.
- Weka namba ya kampuni ya UTT AMIS: 800100.
- Weka namba ya kumbukumbu (Akaunti ya mfuko).
- Weka kiasi.
- Thibitisha kwa kuweka namba yako ya siri ya Airtel Money.
Jinsi ya Kununua Kupitia Benki
4. CRDB Bank
UTT AMIS imeshirikiana rasmi na CRDB kuwezesha wawekezaji kununua vipande kupitia matawi yao au simu:
Kupitia SimBanking (Simu):
- Piga 15003#.
- Chagua Huduma za kifedha.
- Chagua Lipa Bili, kisha fuata hatua kuchagua UTT AMIS.
- Weka kumbukumbu namba (ya akaunti ya mfuko).
- Thibitisha na malipo yatatumwa moja kwa moja UTT.
Kupitia Tawi la Benki: Nenda kwenye tawi lolote la CRDB na:
- Mwambie unataka kununua vipande vya UTT.
- Wape namba ya mfuko wako.
- Lipia kiasi unachotaka kuwekeza.
- Utapewa risiti kama uthibitisho.
5. NMB Bank
NMB pia ni benki mshirika ya UTT AMIS. Unaweza kufanya malipo kupitia:
i. Tawi la NMB:
- Tembelea tawi la karibu.
- Toa taarifa zako za mfuko (jina na namba ya akaunti ya uwekezaji).
- Weka kiasi unachotaka kuwekeza.
- Malipo yatafanyika na utapokea risiti.
ii. NMB Mobile (NMB Mkononi):
- Fungua app au piga *150*66#.
- Chagua Lipa Bili, kisha tafuta au andika UTT AMIS.
- Weka namba ya kumbukumbu.
- Weka kiasi na thibitisha kwa namba ya siri.
Kununua vipande vya UTT AMIS ni rahisi zaidi kuliko wengi wanavyodhani. Ukiwa na simu au ukifika benki, unaweza kuwekeza kwa kiasi chochote kuanzia vipande 10 tu. Hii ni njia salama na ya kuaminika ya kujenga mustakabali wa kifedha.
Soma pia: Bei ya Vipande vya UTT AMIS