Azam TV ni moja kati ya huduma bora za televisheni kwa njia ya king’amuzi nchini Tanzania, inayotoa chaneli mbalimbali za michezo, habari, burudani na tamthilia. Ili kuendelea kufurahia huduma hii bila kukatizwa, ni muhimu kuhakikisha unalipia kifurushi chako kwa wakati.
Zifuatazo ni hatua rahisi za kulipia Azam TV kwa kutumia simu kupitia mitandao tofauti ya malipo.
Jinsi ya Kulipia kwa Simu
Jinsi Ya Kulipia Azam TV kwa YAS
- Piga *150*01# kwenye simu yako.
- Chagua “Lipa Bili.”
- Chagua “Ingiza namba ya biashara.”
- Chagua namba 5 – “King’amuzi (TV Subscription).”
- Chagua “Azam Pay TV.”
- Ingiza namba yako ya akaunti ya Azam TV.
- Ingiza kiasi cha kulipia.
- Ingiza namba ya siri kuthibitisha malipo.
Jinsi Ya Kulipia Azam TV kwa M-Pesa
- Piga *150*00# kwenye simu yako.
- Chagua “Lipa kwa M-Pesa.”
- Chagua “Chagua biashara.”
- Chagua “TV Subscription.”
- Chagua “Azam TV.”
- Ingiza namba yako ya akaunti ya Azam TV.
- Ingiza kiasi cha kulipia.
- Ingiza namba ya siri kuthibitisha malipo.
Jinsi Ya Kulipia Azam TV kwa Airtel Money
- Piga *150*60# kwenye simu yako.
- Chagua “Lipa Bili.”
- Chagua “Ingiza namba ya biashara.”
- Chagua namba 5 – “King’amuzi (TV Subscription).”
- Chagua “Azam.”
- Ingiza namba yako ya akaunti ya Azam TV.
- Ingiza kiasi cha kulipia.
- Ingiza namba ya siri kuthibitisha malipo.
Soma pia: