Young Africans Sports Club, maarufu kama Yanga SC, ni moja ya vilabu vya soka vya kihistoria na vyenye mafanikio makubwa nchini Tanzania. Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1935, Yanga imekuwa chachu ya ushindani mkubwa katika soka la Tanzania, hususan kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Kupitia makala hii, tutaangazia mafanikio ya Yanga SC kwenye ligi hiyo, hususan idadi ya makombe ambayo klabu hiyo imetwaa tangu kuanzishwa kwake.
Safari ya Mafanikio: Makombe 30 Tangu 1935
Kufikia mwisho wa msimu wa 2023/2024, Yanga SC ilikuwa tayari imetwaa mataji 30 ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Hii inaifanya kuwa klabu yenye idadi kubwa zaidi ya mataji ya ligi nchini. Rekodi hii imejengwa kwa miaka mingi ya nidhamu, uwekezaji katika vipaji, na uongozi madhubuti.
Miongoni mwa mafanikio haya, mataji matatu ya hivi karibuni yalipatikana mfululizo katika misimu ya:
- 2021/2022
- 2022/2023
- 2023/2024
Hii inaonyesha uimara wa kikosi cha sasa na uwezo wa Yanga SC kuendelea kuwa tishio kwenye soka la Tanzania.
Idadi ya makombe ya yanga tangu 1935
Klabu ya yanga tangu ianzishwe imetimiza makombe 30 huku ikiipiku klabu pinzani simba sc, ifuatavyo ni misimu na kombe waliochukua yanga sc:
Idadi | Misimu Ya Ubingwa |
30 | 2023/2024 |
28 | 2022-23 |
27 | 2021–22 |
26 | 2016–17 |
25 | 2015–16 |
24 | 2014–15 |
23 | 2012–13 |
22 | 2010–11 |
21 | 2008–09 |
20 | 2007–08 |
19 | 2006 |
18 | 2005 |
17 | 2002 |
16 | 1997 |
15 | 1996 |
14 | 1993 |
13 | 1992 |
12 | 1991 |
11 | 1989 |
10 | 1987 |
9 | 1985 |
8 | 1983 |
7 | 1981 |
6 | 1974 |
5 | 1972 |
4 | 1971 |
3 | 1970 |
2 | 1969 |
1 | 1968 |