Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatarajiwa kutangaza majina ya waombaji waliopata mikopo kwa mwaka wa masomo 2025-2026 Mwisho mwa mwezi huu wa tisa. Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita na waliotuma maombi ya mkopo kupitia mfumo rasmi wa HESLB wanashauriwa kuendelea kufuatilia taarifa kutoka kwa bodi hiyo kupitia tovuti yao rasmi na mitandao ya kijamii.
Majina hayo yatatolewa kwa awamu mbalimbali, kulingana na hatua ya uhakiki wa taarifa na tathmini ya vigezo vya waombaji.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka HESLB, bodi hiyo inatarajia kutoa majina ya awamu ya kwanza (Batch ya Kwanza) mwanzoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu. Hii itawapa nafasi waombaji waliokidhi vigezo kujiandaa mapema kwa ajili ya kuanza masomo yao ya elimu ya juu.
HESLB pia itaendelea kutoa orodha za awamu zinazofuata kwa wale ambao maombi yao yatakuwa yanashughulikiwa katika kipindi hicho. Waombaji wanakumbushwa kuwa na subira na kuhakikisha wanahifadhi taarifa zao muhimu za kuingia kwenye mfumo wa maombi (OLAMS) ili waweze kufuatilia matokeo yao mara yatakapotangazwa.