Soma hapa Bei mpya ya Mafuta aina ya Petrol, Diesel na mafuta ya Taa (Kerosen). Katika hatua inayowalenga watumiaji wa nishati nchini, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Juni 2025. Bei hizi zitaanza kutumika rasmi kuanzia Jumatano, Juni 4, 2025, na zinategemea mabadiliko katika soko la kimataifa la mafuta, mabadiliko ya viwango vya kubadilisha fedha, na gharama za uagizaji mafuta (premiums).
Bei za Mafuta kwa Juni 2025
Kwa mujibu wa EWURA, bei za mafuta kwa mwezi Juni 2025 ni kama ifuatavyo:
Kwa Dar es salaam bei ya mafuta itakuwa kama ifuatavyo
- Petroli: Lita moja itauzwa kwa Tsh 2,885 jijini Dar es Salaam
- Dizeli: Bei mpya ni Tsh2,826 kwa lita moja.
- Mafuta ya Taa (Kerosene): Bei mpya Tsh 2,877 kwa lita moja.
Kwa Bandari ya Tanga bei mpya ya Mafuta itakuwa kama ifuatavyo:
- Petroli: Lita moja itauzwa kwa Tsh 2,946.
- Dizeli: Bei mpya ni Tsh2,887 kwa lita moja.
- Mafuta ya Taa (Kerosene): Bei mpya Tsh 2,938 kwa lita moja.
Na kwa Mtwara mafuta yatauzwa:
- Petroli: Lita moja itauzwa kwa Tsh 2,978.
- Dizeli: Bei mpya ni Tsh2,918 kwa lita moja.
- Mafuta ya Taa (Kerosene): Bei mpya Tsh 2,969 kwa lita moja.
Soma pia: