Serikali imetangaza Nafasi mpya za kazi za walimu 3,500 kwa mwaka 2025 kupitia MDAs na LGAs kwa lengo la kuongeza nguvu kazi katika shule za msingi na sekondari nchini. Ajira hizi ni sehemu ya juhudi endelevu za serikali katika kuboresha sekta ya elimu na kupunguza tatizo la upungufu wa walimu katika maeneo mbalimbali ya nchi. Walimu watakaopangiwa kupitia MDAs na LGAs watachangia katika kuinua ubora wa elimu kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora katika mazingira salama na yenye ufanisi. Serikali imesisitiza kuwa mchakato huu unalenga kuhakikisha usawa wa upatikanaji wa walimu katika kila mkoa na halmashauri nchini.
Bonyeza hapa kupata Tangazo la Nafasi mpya za kazi walimu
Soma pia: Nafasi 17,710 za kazi Kutoka MDAs & LGAs, October 2025