Ada na Gharama za kusoma CPA ni moja ya maswali yanayoulizwa sana na wanafunzi wanaotaka kuanza safari ya kuwa wataalamu wa ukaguzi wa hesabu na uhasibu nchini Tanzania. Ili kuelewa vizuri mchakato wa kujiunga, kulipa ada, kufanya mitihani na kusonga hatua hadi hatua, ni muhimu kufahamu viwango vya ada vinavyotolewa na NBAA.
Mchanganuo wa Ada na Gharama za kusoma CPA kwa Mwaka
Nimekusanya ada zote muhimu—kutoka usajili, mitihani, vitabu, mpaka faini na huduma mbalimbali—ili kukusaidia kupanga bajeti yako vizuri kabla ya kuanza masomo.
1. Ada za Mitihani na Vitabu (Somo Moja)
Kwa wanafunzi wanaopanga kufanya CPA, mojawapo ya gharama muhimu ni ada za mitihani pamoja na vitabu.
- Kitabu Hatua ya ATEC: Tsh 30,000
- Kitabu Hatua ya Kitaaluma (Professional): Tsh 40,000
- NB: Ukirudia somo huto lipia kitabu.
Ada za mitihani kwa kila hatua:
| Hatua | Ada ya Kawaida | Kurudia Somo |
|---|---|---|
| ATEC I | 55,000 | 25,000 |
| ATEC II | 60,000 | 30,000 |
| Foundation | 100,000 | 60,000 |
| Intermediate | 130,000 | 90,000 |
| Final Level | 150,000 | 110,000 |
Kwa wanafunzi wanaotafuta kujua kwa undani Ada na Gharama za kusoma CPA, jedwali hili ndiyo msingi muhimu wa kupanga bajeti ya mitihani ya hatua zote.
2. Ada za Msamaha (Exemption Fees)
Kulingana na sifa za mwanafunzi, unaweza kuomba msamaha wa baadhi ya masomo. Viwango ni kama ifuatavyo (kwa somo moja):
- ATEC I: Tsh 15,000
- ATEC II: Tsh 20,000
- Foundation: Tsh 30,000
3. Ada ya Usajili kwa Kila Hatua ya Mtihani
Katika kujua Ada na Gharama za kusoma CPA, usajili ni sehemu muhimu. Hapa chini ni muhtasari wa ada zote kwa kila level:
ATEC I
- Ada ya fomu – 20,000
- Usajili – 25,000
- Mchango wa mwaka – 35,000
- Jumla: 80,000
ATEC II
- Ada ya fomu – 20,000
- Usajili – 25,000
- Ada ya msamaha – 45,000
- Mchango wa mwaka – 35,000
- Jumla: 125,000
Foundation
- Ada ya fomu – 20,000
- Usajili – 50,000
- Ada ya msamaha – 105,000
- Mchango wa mwaka – 70,000
- Jumla: 245,000
Intermediate
- Ada ya fomu – 20,000
- Usajili – 50,000
- Ada ya msamaha – 205,000
- Mchango wa mwaka – 70,000
- Jumla: 345,000
4. Michango ya Mwaka
- ATEC: Tsh 35,000
- Taaluma (Professional Level): Tsh 70,000
5. Huduma Nyingine na Gharama Zake
Huduma hizi zinaweza kutokea wakati wowote katika safari yako ya CPA, hivyo ni sehemu ya muhimu ya Ada na Gharama za kusoma CPA:
- Transcript: ATEC 35,000 | Professional 40,000
- Barua ya utambuzi: 10,000
- Kitambulisho kilichopotea: 20,000
- Uhakiki wa cheti: 20,000
- Barua ya matokeo: 15,000
- Kukata rufaa kwa somo: 160,000
- Ada ya utafutaji: 25,000
- Jalada la cheti: 20,000
- Uchelewaji wa kuchukua cheti: 20,000 (ikizidi miezi 6)
6. Gharama za Mitihani ya Muhula wa Kati
- A5 Business Law: 450,000
- B4 Public Finance & Taxation I: 500,000
- C4 Public Finance & Taxation II: 550,000
7. Ada kwa Raia wa Kigeni
Raia wa kigeni hulipa mara mbili ya ada za Mtanzania, isipokuwa kwa mitihani ya muhula wa kati. Malipo hufanywa kwa Dola za Marekani.
8. Faini kwa Maombi ya Kuchelewa
| Kiwango cha Faini | Mitihani ya Mei | Mitihani ya Novemba |
|---|---|---|
| 50% Fine | 16 – 28 Februari | 16 – 31 Agosti |
| 100% Fine | 1 – 15 Machi | 1 – 15 Septemba |
Kuelewa Ada na Gharama za kusoma CPA ni hatua muhimu sana kabla ya kuanza safari ya uhasibu. Kwa kujua ada za usajili, mitihani, vitabu, huduma mbalimbali na hata faini, unaweza kupanga bajeti vizuri na kuhakikisha unasoma bila vikwazo. Ada zinaweza kuonekana nyingi, lakini CPA ni moja ya vyeti vyenye thamani kubwa sokoni, na uwekezaji huu unalipa mara dufu baada ya kuhitimu.
Soma pia: