Mashabiki wa soka nchini wanajiandaa kushuhudia pambano kali la hatua ya ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika CAF Champions League kati ya Simba SC na Petro de Luanda kutoka Angola. Mchezo huu unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi kutokana na historia ya timu hizi na umuhimu wake katika kuwania nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano ya kimataifa.
Kwa mashabiki wanaotarajia kufika uwanjani kushuhudia mchezo huu, viingilio rasmi vimetangazwa na vinaonyesha kuwa kuna chaguo kwa kila aina ya shabiki—kuanzia wenzi wa mzunguko hadi mashabiki wa VIP wa juu kabisa.
Viingilio Rasmi vya Mechi ya Simba vs Petro de Luanda
1. Mzunguko (Regular Stands)
Hii ndiyo sehemu yenye idadi kubwa ya mashabiki na imekuwa ikitumiwa sana na wapenzi wa soka wanaopenda shangwe:
- Tsh 5,000
2. VIP Categories
Kwa mashabiki wanaopenda utulivu zaidi na nafasi nzuri ya kutazama mchezo, VIP zimetenganishwa kama ifuatavyo:
- VIP C – Tsh 10,000
- VIP B – Tsh 20,000
- VIP A – Tsh 30,000
3. Premium Seats
Kwa mashabiki wanaopenda huduma za juu zaidi, viti vya Premium vinapatikana kwa bei zifuatazo:
- Platinum – Tsh 150,000
- Tanzanite – Tsh 250,000
Hizi ni sehemu zenye huduma maalumu, mwonekano bora wa uwanja, na mazingira ya kipekee kwa mashabiki wanaotaka kufurahia mechi katika ubora wa juu.
Soma pia: Viingilio Mechi ya Yanga vs AS FAR, CAF Champions League