Jeshi la Magereza leo limetangaza tarehe na vituo vya kufanyia usaili kwa vijana waliochaguliwa kwa mwaka huu 2025. Aidha mkuu wa jeshi la magereza CGP. Jeremia Katungu amesisitiza usaili huo utafanyika kwa vijana waliokidhi vigezo vya Awali tu.
Sambamba na hilo usaili huo utafanyika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza kuanzia tarehe 17 November 2025 hadi tarehe 23 november 2025 na Kwenye ofisi za Magereza za mikoa utafanyika tarehe 17 November 2025. Muda wa usaili huo utaanza saa 2:00 Asubuhi huu wasailiwa wote wanatakiwa kugharamikia gharama za usafiri, chakula na Malazi wao wenyewe.