Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza Second Batch majina ya wanafunzi waliopata mkopo awamu ya pili kwa mwaka wa masomo 2025/2026. Tangazo hili limekuja wiki chache baada ya kutolewa kwa orodha ya awamu ya kwanza, ambapo wanafunzi wengi sasa wamepata matumaini mapya ya kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu bila changamoto za kifedha.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka HESLB, orodha hii ya awamu ya pili inajumuisha wanafunzi waliokuwa wametimiza vigezo vyote vya kupata mkopo lakini hawakuwekwa kwenye orodha ya awamu ya kwanza kutokana na ukaguzi wa taarifa na uhakiki wa nyaraka. Wanafunzi hawa sasa wamepangiwa kiwango cha mkopo kulingana na mahitaji yao na tathmini iliyofanywa na bodi.

Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliopewa Mkopo HESLB 2025/2026 Awamu ya Pili
Ili kuangalia kama umechaguliwa kupata mkopo katika awamu ya pili, fuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti rasmi ya HESLB: www.heslb.go.tz
- Ingia kwenye akaunti yako ya OLAMS: https://olas.heslb.go.tz
- Baada ya kuingia, utapata taarifa kamili kuhusu:
- Kiwango cha mkopo ulichopangiwa
- Gharama ambazo mkopo utazifunika (ada, posho, vitabu n.k.)
- Maelezo ya chuo na kozi uliyochaguliwa
HESLB imeeleza kuwa mchakato wa utoaji mikopo unaendelea, na kwa wale ambao majina yao hayajaonekana bado, orodha ya awamu ya tatu itatangazwa hivi karibuni. Wanafunzi wanashauriwa kuwa wavumilivu na kufuatilia tovuti ya HESLB mara kwa mara kwa taarifa mpya.
Bodi pia imesisitiza kuwa wanafunzi wote waliopata mikopo wanapaswa kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa, ili kuwezesha mfumo wa mikopo kuendelea kusaidia wanafunzi wengine katika miaka ijayo.
Soma pia: Majina ya waliopata Mkopo 2025-2026 – HESLB Loan Beneficiary