Sekretariat ya Utumishi wa Umma (UTUMISHI) kupitia tovuti yake rasmi ya www.ajira.go.tz limetoa orodha ya majina ya waombaji walioitwa kwenye usaili kwa mwaka 2025. Tangazo hili linahusu waombaji wa kazi mbalimbali zilizotangazwa kupitia Ajira Portal kwa taasisi za serikali, ikiwemo MDAs (wizara, idara na wakala wa serikali) pamoja na LGAs (halmashauri za miji na wilaya).
Maelezo Kuhusu Usaili wa UTUMISHI 2025
Kila mwaka, UTUMISHI hutangaza nafasi za kazi kwa niaba ya serikali na taasisi zake mbalimbali. Baada ya mchakato wa maombi kukamilika, orodha ya waliofanikiwa kupangwa kwenye usaili hutolewa kwa uwazi kupitia tovuti rasmi ya Ajira Portal. Mchakato huu unahusisha usaili wa ana kwa ana (oral interview) au kwa njia ya mtandao (online interview), kutegemea aina ya nafasi na idara husika.
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili
Ili kuona kama jina lako limeorodheshwa kwenye usaili wa UTUMISHI 2025, fuata hatua hizi rahisi:
- Fungua tovuti rasmi ya Ajira Portal www.ajira.go.tz
- Bonyeza sehemu ya “Call for Interview” au “Matangazo ya Usaili”
- Pakua PDF yenye orodha ya majina ya walioitwa kwenye usaili
- Tafuta jina lako kwa kutumia Ctrl + F (au “Find” kwenye simu)
- Soma maelekezo ya tarehe, muda, na sehemu ya kufanyia usaili