Leo jioni macho na masikio ya mashabiki wa soka Tanzania na Afrika Mashariki yatakuwa yameelekezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo watani wa jadi, Simba SC na Yanga SC, watakutana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.
Mchezo huu hautakuwa wa kawaida. Ni mwanzo rasmi wa msimu mpya wa soka nchini, na ni fursa kwa kila timu kuonyesha ubabe mapema kabla ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuanza rasmi.
Ngao ya Jamii (Community Shield) ni mechi ya kifahari inayozikutanisha timu zilizofanya vizuri zaidi msimu uliopita. Kwa kawaida, bingwa wa Ligi Kuu hukutana na mshindi wa FA Cup au timu nyingine bora zaidi ikiwa bingwa kapata mataji yote.
Kwa mwaka huu, Simba na Yanga wanakutana tena kutokana na mafanikio yao makubwa msimu uliopita – na hii ni nafasi ya kuanza msimu kwa taji na motisha kubwa.
Saa na Mahali Mechi itachezwa
- Tarehe: Leo – Jumapili, 16 Septemba 2025
- Saa: 11:00 Jioni (Saa za Afrika Mashariki)
- Mahali: Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Uwanja huu wenye uwezo wa zaidi ya mashabiki 60,000 unatarajiwa kujaa kupita kiasi, huku mashabiki kutoka kila kona ya nchi wakimiminika kushuhudia pambano hili la watani wa jadi.
Derby ya Kariakoo haihitaji utangulizi mwingi – ni mechi ya damu, moyo na roho. Leo jioni, historia mpya itaandikwa. Ni Simba au Yanga? Ni nani atakayeondoka na Ngao ya Jamii 2025?
Tuonane saa 11:00 Jioni – Benjamin Mkapa Stadium.
Soma pia: