Baada ya kuchaguliwa kujiunga na moja ya vyuo vya afya vilivyosajiliwa Tanzania, hatua inayofuata ni kupokea Fomu za Kujiunga (Joining Instructions) kutoka chuo husika. Hii ni nyaraka rasmi inayotoa maelekezo ya awali kwa mwanafunzi kabla ya kuanza rasmi masomo ya taaluma ya afya – kama vile Uuguzi, Maabara, Tabibu, Famasi, Radiolojia, na nyinginezo.
Jinsi ya Kupata Fomu ya kujiunga na vyuo vya Afya (Joining Instructions)
- Tembelea Tovuti ya Chuo: Nenda kwenye tovuti rasmi ya chuo unachohitimu.
- Pata Sehemu ya Maelekezo ya Kujiunga: Tafuta sehemu iliyoandikwa “Joining Instructions” au “Admission Letters”.
- Pakua Faili: Bonyeza kwenye kiungo cha kupakua faili ya PDF ya maelekezo ya kujiunga na barua ya kukubaliwa.
- Soma Maelekezo: Hakikisha unasoma kwa makini maelekezo yote yaliyoandikwa ili kufahamu taratibu za kujiunga.
Baada ya mwanafunzi kupokelewa katika chuo cha afya, hupatiwa fomu za kujiunga (Joining Instructions) ambazo zinaeleza kwa kina:
- Tarehe ya kuripoti chuoni
- Mahitaji muhimu kama vifaa vya kujifunzia, sare, na ada
- Sheria na taratibu za chuo
- Malipo ya kujiunga na utaratibu wa malazi
Ni muhimu kusoma na kuelewa fomu za kujiunga mapema kabla ya tarehe ya kuripoti. Hii hukusaidia kujiandaa vizuri kwa masomo ya afya na kuepuka usumbufu wa mwanzo.