Kama unataka kuwekeza kwa njia salama, yenye uwazi na faida nzuri, Mfuko wa Uwekezaji wa UTT AMIS ni chaguo bora kwako. Mfuko huu unatoa fursa kwa Watanzania wote kuwekeza kwa kiwango kidogo na kupata gawio la kila mwaka. Katika makala hii, tutaelezea hatua kwa hatua jinsi ya kujiunga na UTT AMIS na kuanza safari yako ya uwekezaji.
Chagua Mfuko Unaotaka Kujiunga
UTT AMIS inatoa mifuko mbalimbali ya uwekezaji inayolingana na malengo yako. Baadhi ya mifuko hiyo ni:
- Mfuko wa Umoja: Mfuko huu unawekeza katika masoko ya mitaji kama vile hisa zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam na masoko mengine ya fedha. Kiwango cha chini cha kuwekeza ni shilingi 6,500.
- Mfuko wa Wekeza Maisha: Mfuko huu unatoa faida za uwekezaji pamoja na bima ya maisha, ajali, ulemavu wa kudumu na gharama za mazishi. Mpango huu unadumu kwa miaka 10 na kiwango cha chini cha kuwekeza ni shilingi milioni 1.
- Mfuko wa Watoto Fund: Mfuko huu unalenga kuwekeza kwa manufaa ya watoto hadi kufikia umri wa miaka 18. Kiasi cha chini cha uwekezaji ni shilingi 10,000.
Chagua mfuko unaolingana na malengo yako ya kifedha na uwezo wako wa kuwekeza.

Jinsi ya Kufungua Akaunti ya Uwekezaji
Ili kujiunga na UTT AMIS, unahitaji kufungua akaunti ya uwekezaji. Hii inaweza kufanyika kwa njia mbili:
1. Kupitia SimImvest
SimImvest ni huduma ya kifedha inayotolewa na UTT AMIS kupitia mtandao wa simu. Fuata hatua hizi:
- Piga 15082# kwenye simu yako.
- Chagua lugha unayotaka kutumia.
- Chagua “Fungua Akaunti Mpya”.
- Chagua “Akaunti Binafsi”.
- Jaza jina lako na tarehe ya kuzaliwa kwa muundo DDMMYY.
- Chagua “Umiliki Binafsi”.
- Ingiza jina la mfuko unaotaka kujiunga nao.
- Utapokea ujumbe wa uthibitisho
Baada ya hatua hizi, utakuwa na akaunti ya uwekezaji kupitia SimImvest.
2. Kupitia Fomu ya Maombi
Unaweza pia kufungua akaunti kwa kujaza fomu ya maombi. Fuata hatua hizi:
- Tembelea tovuti rasmi ya UTT AMIS: uttamis.co.tz na pakua fomu ya maombi.
- Jaza fomu hiyo kwa usahihi, ukijaza taarifa za kibinafsi, maelezo ya akaunti, na aina ya mfuko wa uwekezaji unaotaka kujiunga nao.
- Wasilisha fomu hiyo kwa njia moja kati ya hizi:
- Tuma kupitia barua pepe: uwekezaji@uttamis.co.tz.
- Tembelea ofisi za UTT AMIS zilizopo Sukari House, Sokoine Drive / Ohio Street, Dar es Salaam.
- Tembelea tawi lolote la CRDB.
Hakikisha umeambatanisha nakala ya kitambulisho chako na picha ya passport size.
3. Subiri Uthibitisho wa Akaunti
Baada ya kuwasilisha maombi yako, utapokea uthibitisho wa kufunguliwa kwa akaunti yako ya uwekezaji. Akaunti yako itakuwa tayari kwa ajili ya kuweka fedha na kuanza kununua vipande vya uwekezaji kulingana na mfuko uliochagua.
4. Anza Kuwekeza
Mara baada ya akaunti yako kufunguliwa, unaweza kuanza kuwekeza kwa kununua vipande vya mfuko uliochagua. Kiasi cha chini cha kuwekeza kinategemea aina ya mfuko uliojiunga nao. Kwa mfano, Mfuko wa Umoja unahitaji kiwango cha chini cha shilingi 6,500, wakati Mfuko wa Wekeza Maisha unahitaji shilingi milioni 1
Kujiunga na UTT AMIS ni hatua nzuri ya kuanza safari yako ya uwekezaji. Kwa kufuata hatua zilizo.
Soma pia: