Michuano ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu wa 2025/2026 imekuwa yenye ushindani mkubwa, huku timu kutoka mataifa mbalimbali barani zikionesha kiwango cha juu cha soka ili kujihakikishia nafasi katika hatua ya makundi. Katika hatua hiyo ya mchujo, klabu nyingi zilipambana vikali nyumbani na ugenini, zikionesha ubora wa kiufundi, nidhamu ya kimchezo na maandalizi bora ya msimu.
Mechi nyingi zilimalizika kwa matokeo finyu, huku zingine zikiamuliwa kwa mikwaju ya penalti, ishara ya ushindani uliozidi kuongezeka mwaka huu. Hali hii imeonyesha wazi kuwa Kombe la Shirikisho Afrika linazidi kuwa jukwaa muhimu kwa vilabu kutoka bara zima kuonesha uwezo wao na kuendeleza ubora wa soka la Afrika katika ngazi ya klabu.
Orodha ya timu zilizofuzu hatua ya Makundi Kombe la shirikisho CAF Confederation cup) 2025-2026
- Azam fc
- Zamalek sc
- CR Belouizdad
- Wydad Ac
- ZESCO United
- AS Maniema
- USM Alger
- San Pedro
- Singida Black Stars
- Olympique de Safi
- Kaizer Chiefs
- Stellenbosch Fc
- Otoho d’Oyo
- Djoliba
- Nairobi United
- Al Masry
Soma pia: