Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 imeendelea kushika kasi kubwa huku ushindani ukiwa mkali katika hatua ya makundi. Baada ya kumalizika kwa michezo ya makundi, mashabiki wa soka barani Afrika wamepata kufahamu timu zilizofanikiwa kusonga mbele hadi hatua ya 16 bora.
Hatua hii ni muhimu sana kwani huwakutanisha timu bora zaidi zilizoonyesha uwezo, nidhamu na mbinu bora za kiufundi, pamoja na baadhi ya timu zilizofuzu kama best losers kutokana na pointi na magoli waliyojikusanyia.
Soma pia: Msimamo wa Makundi AFCON 2025
Orodha ya timu zilizofuzu hatua ya 16 bora michuano ya AFCON
Timu zifuatazo zimefuzu moja kwa moja kwenda hatua ya 16 bora baada ya kumaliza nafasi za juu katika makundi yao:
- Egypt
- Morocco
- Mali
- Algeria
- South Africa
- Nigeria
- Tunisia
Timu hizi zimeonyesha kiwango kizuri katika hatua ya makundi na zinatajwa kuwa miongoni mwa timu zenye nafasi kubwa ya kufika hatua za juu zaidi za mashindano.
Timu zilizofuzu 16 Best Loser
Mbali na timu zilizofuzu moja kwa moja, mfumo wa AFCON huruhusu baadhi ya timu kufuzu kama best losers kulingana na idadi ya pointi, tofauti ya magoli na vigezo vingine vya ushindani. Katika AFCON 2025, timu iliyofanikiwa kufuzu kupitia nafasi hii ni:
- Tanzania (Taifa Stars)
Kufuzu kwa Tanzania kama best loser ni hatua kubwa na ya kihistoria, inayoonyesha maendeleo ya soka la Taifa Stars katika michuano ya kimataifa. Mashabiki wengi wana matumaini kuwa timu itaendelea kupambana kwa nguvu katika hatua ya 16 bora na kuonyesha soka la ushindani dhidi ya wapinzani wao wakubwa.