Safari ya treni ya mwendokasi (SGR) kati ya Dar es Salaam na Dodoma ni sehemu muhimu ya mradi wa maendeleo ya miundombinu nchini Tanzania. Treni hizi za umeme zinatoa huduma ya usafiri wa haraka, salama, na ya kisasa, zikichukua takribani saa tatu na dakika 25 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma. Hapa chini ni ratiba rasmi ya treni ya SGR kwa mwaka 2025.

Ratiba ya Treni ya Haraka (Express) – Dar es Salaam hadi Dodoma
KITUO | KUONDOKA | KITUO | KUWASILI | KUONDOKA | KITUO | KUWASILI |
DSM | 12:00 Asubuhi | MORO | 1:40 Asubuhi | 1:45 Asubuhi | DODOMA | 3:40 Asubuhi |
DODOMA | 11:15 Jioni | MORO | 1:12 Usiku | 1:17 Usiku | DSM | 2:53 Usiku |
Safari hii ya treni ya haraka inachukua takribani saa tatu na dakika 25, na inasimama katika kituo kimoja tu cha Morogoro kabla ya kufika Dodoma.
Ratiba ya Treni ya Kawaida (Ordinary) – Dar es Salaam hadi Dodoma
KITUO | KUONDOKA | KITUO | KUWASILI | KUONDOKA | KITUO | KUWASILI |
DSM | 3:30 Asubuhi | MORO | 5:15 Asubuhi | 5:20 Asubuhi | DODOMA | 7:25 Mchana |
DODOMA | 8:10 Mchana | MORO | 10:15 Jioni | 10:20 Jioni | DSM | 12:10 Jioni |
Safari ya treni ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni njia bora ya kusafiri kwa usalama, haraka, na kwa gharama nafuu. Kwa ratiba hii ya treni, wasafiri wanaweza kupanga safari zao kwa ufanisi na kufurahia huduma za kisasa zinazotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Mapendekezo ya Mhariri: