Umefanikiwa kupata nafasi ya Kusimamia zoezi la Uchaguzi mkuu 2025? Huu hapa mchanganua wa Malipo na Posho ya Nafasi za kazi na Ajira za Kusimamia Uchaguzi mkuu
Malipo na Posho za Ajira Kusimamia Uchaguzi 2025
Siku ya Uchaguzi Msimamizi wa Kituo atalipwa posho ya Shilingi 70,00/- kwa siku kwa muda wa siku mbili posho ya chakula Shilingi 20,000/= kwa siku moja na nauli Shilingi 20,000/=.
Msimamizi Msaidizi wa Kituo atalipwa posho ya Shilingi 65,00= kwa siku kwa muda wa siku mbili, posho ya chakula Shilingi 20,000/= kwa siku moja na nauli Shilingi 20,000/=
Karani Mwongozaji Wapiga Kura atalipwa posho ya Shilingi 65,000/- kwa siku moja na posho ya chakula Shilingi 20,000/=
Wakati wa mafunzo watendaji wote watalipwa posho ya kiasi cha Shilingi 50,000/- kwa siku na nauli kiasi cha Shillingi 20,000/- kwa kila siku ya mafunzo.
Soma pia: Majina ya Usaili kusimamia uchaguzi 2025 – Tume ya uchaguzi