PDF za walimu wa madaraja yote Daraja III A, Daraja la III B na Daraja la III C walioitwa kazini kupitia Ajira Portal kwa mwaka 2025 – 2026 ni nyaraka rasmi zinazotolewa na Serikali kwa lengo la kuwajulisha waombaji wa ajira ya ualimu waliofanikiwa katika mchakato wa usaili na uteuzi. PDF hizi hubeba majina ya waombaji, namba za usajili, kada husika pamoja na taasisi au maeneo ya kazi waliyopangiwa, na hutolewa kupitia tovuti rasmi ya Ajira Portal ili kuhakikisha uwazi na usahihi wa taarifa.
Waombaji wanashauriwa kupakua na kusoma kwa makini PDF husika ili kufahamu maelekezo muhimu kuhusu kuripoti kazini, tarehe za kuanza kazi, pamoja na nyaraka wanazopaswa kuwasilisha wakati wa kuripoti.