Jeshi la Magereza Tanzania limetangaza nafasi mpya za kazi kwa mwaka 2025, likiwaalika vijana wa Kitanzania waliomaliza elimu ya sekondari, diploma, na hata shahada kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo rasmi wa kielektroniki wa TPS Recruitment Management System (TPSRMS). Tangazo hili limetolewa rasmi mnamo Agosti 15, 2025, na dirisha la maombi litakuwa wazi hadi Agosti 29, 2025. Fursa hizi zimefunguliwa kwa nia ya kuimarisha utendaji wa Jeshi la Magereza kwa kuajiri watumishi wapya katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, TEHAMA, utawala, uhasibu, sheria, na huduma za kijamii.
BONYEZA HAPA KUPAKUA TANGAZO LA NAFASI YA AJIRA JESHI LA MAGEREZA
Miongoni mwa masharti ya kuomba nafasi hizi ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania, kuwa na afya njema, tabia njema, kutokuwa na rekodi ya makosa ya jinai, na kufikia vigezo vya umri vilivyowekwa (kati ya miaka 18 hadi 25 kwa waliomaliza kidato cha nne, na hadi miaka 30 kwa wenye taaluma maalum). Aidha, waombaji wote wanatakiwa wawe tayari kufuata mafunzo ya kijeshi na kufanya kazi mahali popote nchini. Mfumo wa maombi wa mtandaoni umeanzishwa ili kurahisisha mchakato wa kuwasilisha maombi, kuimarisha uwazi, na kupunguza mianya ya rushwa katika mchakato wa ajira.