Nafasi za Afisa uchunguzi (Investigation Officer) 250 kutoka TAKUKURU PCCB, vigezo pamoja na mahitaji yote kama ifuatavyo:
Muombaji awe na angalau elimu ya shahada ya kwanza iliyotolewa na chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika moja ya fani zifuatazo: Uhasibu, Usimamizi wa Biashara, Usanifu wa Majengo, Ukadiriji wa Majengo (Quantity Surveying), Uhandisi wa Usindikaji wa Kemikali, Maendeleo ya Jamii, Sayansi ya Kompyuta/TEHAMA, Uhandisi wa Ujenzi, Uchumi na Mipango, Uhandisi wa Umeme, Lishe na Sayansi ya Chakula. Usimamizi wa Rasilimali Watu. Usimamizi na Tathmini ya Ardhi, Sheria, Uhandisi wa Mitambo, Uhandisi wa Mafuta na Gesi, Ununuzi na Ugavi, Usimamizi wa Miradi, Ushauri Nasaha, Utawala wa Umma, Mahusiano ya Umma/Mawasiliano ya Umma, Usimamizi wa Kumbukumbu, Sayansi ya Michezo/Elimu ya Viungo, Takwimu, na Uhandisi wa Maji.
- Muombaji awe na ufaulu wa kuanzia daraja la pili la chini (lower second class).
- Waombaji waliosajiliwa na Bodi za Kitaaluma watapewa kipaumbele zaidi.
Sifa zingine:
- Waombaji wasiwe wamefika umri wa miaka 29 kufikia May, 2026
Maombi yote yanatumwa online bonyeza hapa