Idara ya Uhamiaji imetangaza nafasi mpya za kazi 2025 kwa Watanzania wenye sifa mbalimbali, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za uhamiaji nchini. Nafasi hizi zinahusisha kada tofauti kulingana na mahitaji ya idara, zikiwemo nafasi za kiutawala, kiusalama na kitaalamu, huku waombaji wakitakiwa kuwa na elimu inayokidhi vigezo vilivyotangazwa, afya njema na nidhamu ya hali ya juu.
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI ZA KAZI JESHI LA UHAMIAJI
- Awe ni raia wa Tanzania;
- Awe hana ajira au hajawahi kuajiriwa na Taasisi yoyote Serikalini;
- Awe na Cheti cha Kuzaliwa;
- Awe na Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho iliyotolewa na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)
- Awe na siha njema ya mwili na akili.
- Awe hajawahi kutumia Dawa za kulevya;
- Asiwe na kumbukumbu au taarifa zozote za kuhusika katika masuala au matukio ya uhalifu au jinai;
- Asiwe na alama yoyote au michoro (Tatoo) katika mwili wake;
- Awe hajaoa au kuolewa wala kuwa na mtoto;
- Mwombaji mwenye Elimu ya Kidato cha Nne awe na sifa kuanzia Daraja la kwanza (1) mpaka Daraja la tatu (3) na awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 22, Mwombaji mwenye Astashahada na Stashahada awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 25 na Mwombaji mwenye Elimu ya Shahada/Stashahada ya Juu awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 30.
- Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya Kijeshi ya Uhamiaji.
- Awe tayari kufanya kazi za Idara ya Uhamiaji mahali popote Tanzania.
- Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za ufuatiliaji na uendeshwaji wa zoezi la Ajira.
MAOMBI YATAKAYOPEWA KIPAUMBELE:
Maombi yatakayopewa kipaumbele ni ya waombaji wenye taaluma ngazi ya Shahada/Stashahada ya Juu, Stashahada na Astashahada kutoka katika Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali wenye fani zifuatazo:- Mtaalamu wa Lugha za Kimataifa, Utawala, Sheria, Uhusiano, TEHAMA(Cyber Security,Database Developer,System Developer,Artifical Intelligence and Machine Learning), Masijala, Ukatibu Mahsusi, Uhasibu, Ununuzi na Ugavi waliosajiliwa na Bodi, Takwimu, Uchumi, Umeme, Ufundi wa AC, Brass band, Wataalamu wa Saikolojia (Psychology) na Mpiga chapa (Printer). Pia waombaji wenye ujuzi wa Ufundi wa Magari na Udereva watapewa kipaumbele.
NAMNA YA KUFANYA MAOMBI:
Maombi yote ya ajira yatawasilishwa kupitia tovuti ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni https://www.immigration.go.tz kuanzia tarehe 29 Desemba, 2025 na mwisho wa kufanya maombi ni tarehe 11 Januari, 2026. Wakati wa kufanya maombi, mwombaji anatakiwa kuambatisha (upload) kwenye
mfumo wa ajira nyaraka zifuatazo zilizo katika mfumo wa PDF (kila Nyaraka moja isizidi 300Kb);
✓ Picha (passport size) ya hivi karibuni iliyo katika mfumo wa jpg/png isiyozidi 300Kb kwa ajili ya kuambatisha kwenye mfumo (upload);
✓ Barua ya maombi ya ajira iliyoandikwa kwa mkono;
✓ Barua ya utambulisho toka Serikali ya Mtaa/Kijiji au Shehia; kwa walio Makambini JKT/JKU wawe na barua za utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Kambi;
✓ Cheti cha kuzaliwa;
✓ Awe na Kitambulisho cha Taifa (NIDA) au namba ya NIDA kwa ajili ya kujisajili kwenye mfumo;
✓ Awe na Index namba za vyeti vya kufaulu Kidato cha Nne na Kidato cha Sita ambazo atajaza kwenye mfumo wa ajira;
✓ Awe na namba ya utambuzi ya cheti cha ngazi ya Astashahada, Stashahada, na Shahada/Stashahada ya juu inayotambuliwa na TCU au NACTVET ambayo atajaza namba hiyo kwenye mfumo wa ajira;
✓ Vyeti vya usajili wa taaluma kwa fani zinazohitaji usajili wa Bodi;
✓ Wasifu wa mwombaji (CV).
✓ Aidha, changamoto/maulizo wasilisha kupitia: ajira@immigration.go.tz
Soma pia:
1 Comment
MIMI NAITES JACKSON NDARO MASAKA NI KIJANA MWENYE UMRI WA MIAKA 24 NINAISHI MWANZA NAPENDA SANA KULITUMIKIA TAIFA LANGU KWA NAFASI YA JESHI LA UHAMIAJI ENDAPO NITAKUBALIWA WAKO MTIIFU
JACKSON NDARO MASAKA