Serikali imetangaza nafasi 292 za ajira za Afisa Kilimo Msaidizi (Agricultural Field Officer) kupitia MDAs na LGAs kwa mwaka 2025, zikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha sekta ya kilimo nchini. Nafasi hizi zimeelekezwa kwa wataalamu watakaosaidia katika kutoa elimu kwa wakulima, kusimamia uzalishaji bora wa mazao, na kuhakikisha matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo. Kupitia ajira hizi, serikali inalenga kuongeza tija ya kilimo, kuboresha kipato cha wakulima, na kuchochea maendeleo ya uchumi wa vijijini.
Soma pia: