Katika juhudi za kuinua maisha ya wananchi kiuchumi, halmashauri nyingi nchini Tanzania zimekuwa zikitenga asilimia ya mapato yao kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu.
Mikopo hii hutolewa bila riba, na inalenga kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi. Ili kupata mkopo huu, kikundi au mwombaji binafsi anatakiwa kuandika barua rasmi ya maombi.
Katika makala hii, tutakuonesha mfano wa barua ya kuomba mkopo halmashauri, pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuwasilisha maombi yako.
Nani Anaweza Kuomba Mkopo wa Halmashauri?
Kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Serikali za Mitaa:
- Vikundi vya vijana (wenye umri wa miaka 18–35)
- Vikundi vya wanawake
- Vikundi vya watu wenye ulemavu
Kikundi kinatakiwa kuwa kimesajiliwa, kina akaunti ya benki, na kiwe na mpango wa biashara (business plan) unaoeleweka.
Mambo Muhimu ya Kuweka Kwenye Barua ya Maombi ya Mkopo
- Jina la kikundi chenu na anuani rasmi
- Tarehe ya kuandika barua
- Anuani ya halmashauri mnayoomba mkopo
- Kichwa cha habari (RE: Maombi ya Mkopo…)
- Utambulisho mfupi wa kikundi
- Kiasi cha mkopo mnaoomba
- Lengo la mkopo na matumizi yake
- Viambatisho (nakala ya cheti cha usajili, business plan, picha ya wanachama, nk.)
- Sahihi za viongozi wa kikundi
Mfano wa Barua ya Kuomba Mkopo Halmashauri
Kikundi cha Vijana Wajasiriamali – Tumaini
S.L.P 255,
Mlandizi,
Mkoa wa Pwani.23 Agosti 2025
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha
S.L.P 789,
Kibaha.YAH: MAOMBI YA MKOPO KUTOKA MFUKO WA 10% YA HALMASHAURI
Ndugu Mkurugenzi,
Kupitia barua hii, sisi kikundi cha Tumaini, kilichosajiliwa rasmi tarehe 15 Januari 2024 kwa namba KJN/VC/1245, tunaomba kupewa mkopo kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya vijana.
Kikundi chetu kina jumla ya wanachama saba (7), wote wakiwa vijana wenye umri kati ya miaka 20 hadi 30.
Tunaiomba halmashauri itupatie mkopo wa shilingi TSh 5,000,000 kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa mayai katika kata ya Mwendapole.
Tumeambatanisha business plan ya mradi wetu, nakala ya cheti cha usajili, picha za wanachama na taarifa ya benki. Tunaamini kuwa mradi huu utasaidia kikundi kujitegemea kiuchumi na kuchangia maendeleo ya kata yetu.
Tunashukuru kwa fursa hii na tunasubiri majibu kutoka kwenu kwa matumaini makubwa.
Wako kwa ushirikiano,
Jane Amani
Mwenyekiti – Kikundi cha TumainiPeter Joseph
KatibuAsha Selemani
Mhasibu
Kuandika barua ya kuomba mkopo halmashauri ni hatua muhimu katika kupata fedha za kuendeleza miradi ya vijana, wanawake au watu wenye ulemavu. Hakikisha barua yako imeandikwa kwa lugha rasmi, ina maelezo sahihi na nyaraka zote muhimu zimeambatanishwa.
Ikiwa unahitaji msaada zaidi katika kuandaa mpango wa biashara au nyaraka nyingine za kuambatanisha, unaweza kufika ofisi ya maendeleo ya jamii ya kata au halmashauri yako.
Soma pia: