Leo Jumamosi Mechi za Marudiano za mkondo wa pili wa hatua ya awali Klabu Bingwa na Kombe la shirikisho CAF. Baada ya mechi za mkondo wa kwanza kukamilika leo hii Baadhi ya timu za Tanzania Bara zinashuka tena dimbani kumenyana awamu ya pili.
Mechi kubwa inayosubiriwa kwa hamu katika mzunguko huu wa pili ni kati ya yanga sc na Silver Strikers, Ni baada ya mkondo wa kwanza timu ya wananchi yanga sc kuchezea kichapo cha bao moja kwa sufuri na kupelekea kufukuzwa kwa kocha wao mkuu Roma Folz, wanachama pamoja na mashabiki wa Yanga wanahamu kubwa ya kushuhudia mechi iyo wakiwa na lengo moja tu la kufuzu na kuingia makundi ya klabu bingwa Mwaka huu.
Ikumbukwe watani wao wa jadi simba sc wao tayari wameshaingiza mguu mmoja hatua ya makundi ya klabu bingwa baada ya kutoka na ushindi wa mabao matatu kwa sufuri katika mechi ya mkondo wa kwanza.
Je wananchi wataweza kupindua meza na kufuzu mechi hiyo?, Hili ni fumbo kila mdau wa soka anatamani kuona likifumbuliwa na wananchi.
Soma pia: Wachezaji wanaowania Tuzo za CAF (Interclub Player) msimu wa 2025