Usafiri kati ya Dar es Salaam na Morogoro ni miongoni mwa ruti maarufu zaidi nchini Tanzania. Kwa wale wanaotafuta usafiri wa haraka, nafuu na wa uhakika, mabasi ya Dar to Morogoro ni chaguo bora. Katika makala hii, utapata maelezo kamili kuhusu ratiba, bei za nauli, vituo vikuu na vidokezo vya kusafiri kwa urahisi.
Contents
Aina ya Mabasi Yanayofanya Safari Dar es Salaam hadi Morogoro
Kuna aina mbalimbali za mabasi yanayotoa huduma hii, ikiwa ni pamoja na:
- Mabasi ya kawaida (Normal class) – mfano: Abood, Happy Nation
- Mabasi ya semi-luxury na luxury – mfano: BM Luxury, New Force, Msolwa Executive
Mabasi haya huanza safari kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni, na muda wa safari ni takribani masaa 3 hadi 5 kutegemea na foleni au hali ya barabara.
Nauli za Mabasi Dar to Morogoro
Nauli inategemea aina ya basi na huduma zake. Kwa ujumla:
- Mabasi ya kawaida: Tsh 6,000 – 8,000
- Semi-luxury: Tsh 10,000 – 12,000
- Luxury: Tsh 15,000 – 18,000
Vidokezo Muhimu:
- Weka tiketi mapema, hasa wikiendi au msimu wa sikukuu
- Beba vitambulisho halali kwa ajili ya usalama na usajili wa abiria
- Angalia kama basi lina AC, charging ports au huduma ya Wi-Fi kabla ya kuchagua
Vituo Vikuu vya Mabasi ya Dar to morogoro
Dar es Salaam:
- Ubungo Bus Terminal (UBT)
- Mbagala (kwa baadhi ya mabasi ya mikoani)
Morogoro:
- Msamvu Bus Terminal
Sababu za Kuchagua Mabasi Badala ya Gari Binafsi
- Gharama nafuu
- Hupunguza uchovu wa kuendesha mwenyewe
- Upatikanaji wa ratiba nyingi kwa siku.
Mapendekezo ya Mhariri: