Msimu wa 2024/2025 umekuwa wa kuvutia sana katika soka la Afrika, hasa kwa wapenzi wa soka la Tanzania. Nyota wawili waliowahi kucheza ndani ya NBC Premier League huku Fiston Mayele alikuwa Yanga na Shomari Kapombe akiwa Simba, wamekutana tena – safari hii si kama wachezaji wa timu moja, bali kama wapinzani wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa CAF Interclub 2025.
Baada ya kutamba akiwa na Yanga SC kwa misimu mitatu mfululizo, Fiston Mayele alijiunga na Pyramid FC ya Misri, ambako ameendelea kung’ara katika michuano ya CAF Champions League. Akiwa kinara wa magoli na msaada mkubwa kwa timu yake, Mayele amethibitisha kuwa ubora wake haukuwa tu ndani ya Tanzania bali pia katika ngazi ya bara la Afrika. Uwezo wake wa kumalizia mipira, kasi, na umakini wa kufunga umechangia kumuingiza kwenye orodha ya wachezaji bora wanaowania tuzo ya mwaka huu.
Kwa upande mwingine, Shomari Kapombe ameendeleza ubora wake ndani ya Simba SC, akiibuka kuwa mmoja wa mabeki bora zaidi Afrika Mashariki. Uongozi wake uwanjani, nidhamu na uwezo wa kusaidia mashambulizi vimefanya Simba kuwa na msimu mzuri katika CAF Confederation Cup. Kapombe amekuwa mfano bora wa mchezaji mwenye uzoefu na uthabiti, hali iliyomuweka kwenye orodha hiyo ya heshima ya wachezaji bora wa CAF Interclub.
Wanakutana Tena – Sasa Kwenye Jukwaa la Kihistoria
Kukutana tena kwa Kapombe na Mayele katika kinyang’anyiro hiki cha tuzo ni jambo la kuvutia kwa mashabiki wa soka Tanzania. Wawili hawa wanawakilisha klabu tofauti na huku kila mmoja akibeba bendera ya Nchi yake katika jukwaa la kimataifa. Hii ni dalili kuwa soka la Tanzania linaendelea kukua na kutoa wachezaji wanaoweza kushindana katika viwango vya juu barani Afrika.
Soma pia: Wachezaji wanaowania Tuzo za CAF (Interclub Player) msimu wa 2025